Posted by Esta Malibiche on Sept 1.2016
Aliyekuwa
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mkoani Mwanza, John
Nzwalile (kulia), akirejesha kadi ya chama hicho kwa Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo katika ofisi za
CCM hii leo.
Nzwalile
ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema Taifa, Mjumbe Baraza
Kuu Chadema Taifa, Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano Chadema Mkoa wa
Mwanza, amefikia uamuzi huo baada ya jana kujivua vyeo hivyo.
Amesema
amefikia hatua hiyo kutokana na kwamba Chadema imepoteza mwelekeo kwani
kimekuwa kikiibuka na oparesheni za kuichonganisha serikali na wananchi
huku pia demokrasia ikikosekana ndani ya chama hicho.
"Kama
ni udikiteta basi mimi niseme Chadema ndiko kuna udikiteta kwani zaidi
ya mara tatu nimemsikia Lowasa (Edward Lowasa, aliyekuwa mgombea urais
2015) akisema yeye ndiye mgombea urais mwaka 2020, kwa kikao gani".
Amesema Nzwalile na kuongeza kwamba yale mambo yote mabaya yaliyokuwa
yakifanyika ndani ya CCM yamenyooshwa hivyo hakuna haja ya yeye
kuendelea kukaa Chadema.
Amesema
atazunguka Wilaya zote ili kuhakikisha anawarejesha wengine ndani ya
CCM huku akiwa na jukumu moja la kuubomoa Ukuta unaoelezwa kujengwa na
Chadema kwani ni ukuta wa tope hivyo atatumia tu maji kuubomoa.
Nzwalile
amekaribishwa ndani ya CCM na Mwenyekiti wa Chama hicho mkoani Mwanza,
Dkt.Antony Diallo, ambaye pia amewakaribisha makada wengine wa upinzani
kuhamia CCM akisema kwamba chama hicho kinaendesha mambo yake
kidemokrasia.
Mwenyekiti
wa CCM mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo (kushoto) akipokea kadi ya
Chadema ya aliyekuwa Katibu wa Chadema mkoani Mwanza, John Nzwalile
(katikati).
Mwenyekiti
wa CCM mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo (kushoto) akimkabidhi kadi ya
CCM aliyekuwa Katibu wa Chadema mkoani Mwanza, John Nzwalile (kulia).
Soma HAPA Taarifa ya awali.
0 maoni:
Chapisha Maoni