Jumanne, 27 Septemba 2016

Naibu Waziri wa Afya Dk.Kigwangalla afanya ziara Hospitali za Wilaya ya Mlele na Mpanda Mkoani Katavi


Posted by Esta Malibiche on in NEWS 
 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Mlele na kutembelea Hospitali ya Mlele ya Wilaya hiyo pamoja na Hospitali ya Mpanda iliyopo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi huku akitoa maagizo mbalimbali ya kiutendaji.
Katika ziara yake katika Hospitali ya Mlele, Dk.Kigwangalla amewaagiza viongozi wa Serikali wa Wilaya na ule wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanakamilisha mambo muhimu ikiwemo ujenzi wa chumba cha upasuaji, jengo la kuhifadhia mahiti  na vitu vingine huku akitaka ndani ya miezi mitatu view vimekamilika.
Akiwa katika Hospitali hiyo ya Mlele, Dk.Kigwangalla ameweza kutembelea sehemu mbalimbali za hospitali pamoja na kukagua ujenzi wa majengo ya Chumba cha upasuaji, chumba cha kuhifadhia maiti na majengo mengine ambapo amemtaka Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wanafanya juhudi wanakamilisha kwa wakati majengo hayo ili wananchi wapate huduma bora.
Kwa upande wa ziara yake hiyo katika Wilaya ya Tanganyika yaliyopo makao makuu ya Mkoa wa Katavi, Dk. Kigwangalla ameweza kutembelea Hospitali ya Mpanda ambayo kwa sasa inahudumia kama Hospitali ya Mkoa ambapo napo ameagiza kufanyiwa marekebisho mbalimbali  ikiwemo kuzingatia masuala  usafi.
Aidha, ametoa maagizo kuhakikisha wanafunga mfumo wa malipo wa kisasa katika vyanzo vyote vya mapato ili kukusanya pesa nyingi zaidi zitakazoweza kuendesha huduma za Afya ndani ya Hospitali hiyo.
 Mpanda hospitalNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Chifu Kayamba wa Pili wa Kabila la Wakonongo. Wakati wa kupokelewa alipowasili ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Mlele,Mkoani Katavi.
dsc_0731Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya viongozi na watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Mkoani Katavi.
dsc_0746
Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Bi.Rachel Kasanda akisoma taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati)
dsc_0763Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na watendaji wa Wilaya ya Mlele
dsc_0769Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na madaktari wa hospitali ya Mlele
dsc_0779 dsc_0799
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya vifaa katika chumba cha Maabara ya hospitali ya Mlele
dsc_0801 dsc_0805
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitembelea katika viunga vya hospitali ya Mlele
dsc_0818
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo 
dsc_0833
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na Chifu Kayamba wa pili wa kabila la Wakonongo
dsc_0845
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua jengo la chumba cha Upasuaji wa hospitali ya Mlele
dsc_0850 dsc_0851 dsc_0853Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua jengo linalojengwa la chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Mlele
dsc_0897
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na watumishi wa Hositali ya Mpanda
dsc_0907
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua stoo ya dawa ya hospitali ya Mpanda
dsc_0918
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo katika chumba cha Maabara ya Hospitali ya Mpanda
dsc_0923
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wananchi (Hawapo pichani) wakati wa ziara yake hiyo katika Hospitali ya Mpanda
dsc_0942
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa uongozi wa Hospitali ya Mpanda juu ya kufanyia marekebisho mapungufu yaliyobainika. 
(Picha zote na Andrew Chale,cKatavi).

0 maoni:

Chapisha Maoni