Jumatatu, 13 Juni 2016

Ni vyema jamii kuwatumia viongozi wa dini pamoja na mabaraza ya wazee kutafuta suluhisho la matendo ya hujuma-Suleiman Salum

maxresdefaultNa  Masanja Mabula –Pemba
…………………………………..
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Pemba imewashauri wananchi kuwatumia viongozi wa Dini pamoja na mabaraza ya wazee katika kutafuta suluhisho na matendo ya hujuma yanayoendelea kutokea Kisiwani humo .
Ushauri huo umetolewa na Msaidizi Kamishna wa Tume hiyo Pemba , Suleiman Salum wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko ofisini Kwake na kusema ofisi yake imesikitishwa na matendo hayo .
Amesema kwamba suluhisho na matendo hayo inaweza kupatikana iwapo jamii itawatumia viongozi wa dini pamoja na mabaraza ya wazee katika kutafuta ushauri na suluhisho la matendo   ya kuhujumiwa mali za wananchi .
Aidha amefahamisha kuwa matendo hayo yanakwenye kinyume na msingi ya haki za binadamu na utawala bora kwani yanaweza kusababisha kutowekwa kwa amani ya nchi .
“Ni vyema jamii kuwatumia viongozi wa dini pamoja na mabaraza ya wazee kutafuta suluhisho la matendo ya hujuma yanaendelea kutokea kwa baadhi ya maeneo ya Kisiwani cha Pemba ”alifahamisha.
Akizungumza utendaji kazi wa Tume hiyo Kisiwani hapa , alisema kwamba bado wananchi hawajakuwa na mwamko wa kitumia kwani tangu ilipopfunguliwa Septemba mwaka 2015 , wamepokea lalamiko moja la ukiukwaji wa haki za binadamu .
Pia amefahamisha kuwa licha ya Tume kutoa elimu kupitia Ofisi za wakuu wa Wilaya na Mikoa , lakini bado mwitikio wa wananchi ni mdogo na kutumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuwasilisha malalamiko yao ili yafanyiwe kazi .
“Tunatoa elimu kupitia vyombo vya habari , masheha pamoja na Ofisi za wakuu wa Wilaya na Mikoa , lakini mwitikio bado ni mdogo , hivyo nawaomba sana wananchi waitumia ofisi yetu kuwasilisha malalamiko yao ”alishauri .
Baadhi ya wananchi waliozungumza na mwandishi wa habari hizi , wamesema wanahitaji  elimu juu ya kuitumia Tume hiyo , kuomba watendaji wake kufika maeneo ya vijini kwa ajili ya kutoa elimu .
Hata hivyo  Msaidizi wa Tume hiyo  inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa wafanyakazi jambo ambalo linawakamishwa kuweza kuyafikia maeneo yote ya Kisiwani cha Pemba .

0 maoni:

Chapisha Maoni