Jumapili, 25 Septemba 2016

TIMU YA WABUNGE MASHABIKI WA YANGA YAICHALAZA MAGOLI 5-2 TIMU YA WABUNGE MASHABIKI WA SIMBA UWANJA WA TAIFA LEO

Posted by Esta Malibiche on Sept25.2016

buv1
 Kikosi cha timu ya Wabunge mashabiki wa Yanga kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na Wabunge mashabiki wa Simba ambapo Mashaibiki wabunge wa Yanga wameshinda magoli 5-2 dhidi ya wabunge mashabiki wa Simba katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo jijini Dar es salaam.
Mchezo huo ulikuwa ni kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni Bukoba mkoani Kagera ambapo nyumba na miundombinu iliharibika vibaya huku likipoteza maisha ya watu 17 na kujeruhi wengine wengi.
buv2
Beki wa timu ya Wabunge wa Simba, Wiliam Ngeleja akichuana na mshambuliaji wa Wabunge wa Yanga, Mwigulu Nchemba.
buv3
Mshambuliaji wa timu ya Wabunge mashabiki wa Yanga, Ridhiwan
Kikwete (kushoto), akimtoka beki wa timu ya Wabunge mashabiki wa Simba, Adam Malima katikamchezo wa Matumaini uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
buv4 
 Mashabiki wakifuatilia mchezo huo wakifuatilia kwa karibu wakati ulipokuwa ukiendelea kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.(Picha zote na Francis Dande)
buv5
 Mashabiki wakifuatilia mchezo huo wakifuatilia kwa karibu wakati ulipokuwa ukiendelea kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.(Picha zote na Francis Dande)

0 maoni:

Chapisha Maoni