Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Prof. James Mdoe akielezea
fursa za uwekezaji kwenye sekta ya madini nchini
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Prof. James Mdoe (aliyekaa
mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha mabalozi kutoka katika nchi za
Ujerumani na Denmark pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na
Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) na Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kilichofanyika hivi
karibuni jijini Dar es Salaam
Sehemu ya mabalozi na wawakilishi
kutoka katika nchi za Denmark na Ujerumani wakifuatilia kwa makini
maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Prof. James Mdoe ( hayupo
pichani)
Balozi wa Denmark Nchini, Einar Jensen akieleza jambo katika kikao hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo
(kushoto) na Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Nchini,
James Andelile (kulia) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na
Balozi wa Denmark Nchini, Einar Jensen (hayupo pichani)
Balozi wa Denmark Nchini, Einar
Jensen (kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo
(kulia) kwenye ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es
Salaam.
Balozi wa Denmark Nchini, Einar
Jensen (kushoto) akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati,
Dkt. Juliana Pallangyo jijini Dar es Salaam
Kutoka kulia Balozi wa Denmark
Nchini, Einar Jensen, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo, Mwakilishi kutoka
kampuni ya Ferrostaal Industrial Projects, Wilfried Wiemann na
mwakilishi kutoka Ubalozi wa Denmark, Mette Melson wakiwa katika picha
ya pamoja
……………………………………………………………
Na Greyson Mwase
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Prof. James Mdoe amekutana
na mabalozi kutoka nchi za Ujerumani na Denmark ikiwa ni mwendelezo wa
maandalizi kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha mbolea wilayani Kilwa
mkoani Lindi.
Kiwanda hicho kinatarajiwa
kumilikiwa na kampuni za Ferrostaal Industrial Projects ya Ujerumani,
Haldor Topsoe ya Denmark na Fauji Fertilizer Limited ya Pakinstan
kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC)
Akizungumza katika kikao hicho
kilichokutanisha pia watendaji kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za
Nishati naMaji (EWURA) na TPDC, Balozi wa Denmark Nchini Einar Jensen
alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa kiwanda cha mbolea, Tanzania
itapata manufaa makubwa ikiwa ni pamoja na ajira, fedha za kigeni
kutokana na kuuza mbolea nje ya nchi na hivyo kuinua uchumi wa nchi.
Wakati huohuo Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Prof. James
Mdoe alisema kuwa maandalizi kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho bado
yanaendelea ikiwa ni pamoja na ushirikishwaji wa wadau mbalimbali.
0 maoni:
Chapisha Maoni