Posted by Esta Malibiche on Sept15.2016 in MICHEZO
mkuu
wa wilaya ya mufindi Jumhuri Wiliamu akipiga mpira katika eneo la
penati kuashiria kuwa mashindano ya mgimwa cup yamezinduliwa rasmi
mkuu
wa wilaya mufindi Jumhuri Wiliamu aliyeshika mpira kulia sambamba na
mwenyekiti wa ccm mufindi yohanis kaguo aliyeshika mpira kushoto wakiwa
na baadhi ya wachezajimkuu wa wilaya mufind Jumhuri Wiliamu akikagua timu kabla mtanange kuanza.
mkuu wa wilaya mufind Jumhuri Wiliamu akikagua timu kabla mtanange kuanza huku akiwapa neno wachezaji wa timu husika katika kiwanja cha Ikwea.
…………………………………………………………
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MASHINDANO ya kombe Mgimwa Cup yamezinduliwa rasmi katika kijiji cha Ikwea kata ya Ikwea wilayani mufindi mkoani Iringa kwa kushirikisha timu za vijiji vyote vya jimbo la mfundi kaskazini kwa lengo la kuinua vipaji wa wachezaji wa jimbo hilo.
Akizindua
mashindano hayo yaliyofanyika Kiwanja cha Ikwea katika kijiji cha Ikwea
mkuu wa wilaya JumhuriWiliamu kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la mufindi
kaskazini alisema ni wakati mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya
mchangani kwani yamesheheni vipaji vingi vitakavyosaidia kuendeleza
mpira wa Tanzania wakati ambapo taifa likiendelea kupata matokeo
yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa,
“Mashindano
haya ni muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya
vijana wetu na kuweza kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu
wakati wa michezo hiyo” alisema Wiliamu
Aidha
Wiliamu aliongeza kwa kusema kuwa mpira wa miguu umekuwa na faida kwa
wachezaji kwani wanaweza kujitengezea vyanzo vya ajira kama mbwana
samatta na wachezaji wengine walipwa vizuri saizi hapa nchini hata nje
ya nchi.
“
Soka imewapa ajira mamilioni ya wachezaji na viongozi ulimwenguni na
wameweza kuishi maisha ya kifahari kutokana na mishahara wanayopata”,
alisema Wiliamu
Mwenyekiti
wa Kamati yaMashindano hayo Felix nyimbo aliwataka washiriki wa
mashindano hayo kujituma ili ipatikane timu ya kata ambayo itakuwa
ikiwakilisha kata hiyo katika mashindano ya wilaya, kanda hadi taifa.
“Mwaka
huu tumekuja na wataalamu wanachagua vipaji maalumu kwaajili ya
kujiunga na timu yetu yakurugenzi ya mafinga na lengo likiwa ni
kuhakikisha vipaji vyote vya jimbo la mufindi kaskazini vinaonekana na
vinafika mbali kwa kuwa sasa mpira ni ajira si mnamuana mchezaji Mbwana
Samatta”.alisema nyimbo
Kwa
upande wake mlezi wa mashindano hayo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi
(ccm) wilaya mufindi Yohanes Kaguo alisema ataendelea kwaunganisha
vijana kupitia michezo na kusaidia kukuza mpira wa wilaya ya mufindi.
“Ilani
ya chama cha mapinduzi inatutaka mwenyeviti kote nchini kuhakikisha
michezo inafanyika mara kwa mara na kuleta tija kwa taifa ili tuondokane
kuwa kuwa vichwa vya wendawazimu”alisema kaguo.
Mashindano
ya mgimwa Cup ni miongoni mwa mashindano yanayolenga kuibua vipaji vya
vijana vijijini ili kuwawezesha kupata nafasi ya kucheza katika vilabu
vikubwa nchini.
0 maoni:
Chapisha Maoni