Kama ulishawahi fikiri kujisaidia kwenye choo kilichotengenezwa kwa dhahabu huu ndo wasaa mzuri wa kutimiza ndoto yako.
Makumbusho
ya sanaa maruufu jijini New York ijulikanayo kwa jina Guggenheim
imekizindua choo maalum kilichopewa jina la ‘America’ katika moja ya
vyoo vingi vilivyopo katika makumbusho hiyo.
Maurizio
Cattelan (55) mzaliwa wa nchini Italia ndie mbunifu wa choo hicho
kilichotengenezwa kwa dhahabu na ameripotiwa na waandishi wa habari wa
nchini Marekani akisema kuwa choo hicho kina dhamira nyingi lakini moja
wapo ni kuonesha kukosekana kwa usawa wa kiuchumi duniani.
Si
mara ya kwanza kwa taswira ya choo kutumika katika sanaa, mnamo mwaka
1917 msanii Marcel Duchamp alitengeneza mfano wa choo cha ukuta maarufu
kwa jina la ‘fountain’ ambacho kilileta mabadiliko makubwa kwenye jamii
ya sanaa.
Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC).
Mbunifu wa choo hicho Maurizio Cattelan
0 maoni:
Chapisha Maoni