Jumatano, 14 Septemba 2016

DC IRINGA RICHARD KASESELA AFUNGUA MAFUNZO YA MGAMBO

Posted by EstaMalibiche on Sept.14 2016 in News


Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amefungua  mafunzo ya Mgambo Kata ya Wasa na  Kihanga Halmashauri ya Iringa.
Katika mafunzo hayo,takribani mgambo 170 wameanza rasmi mafunzo hayo pamoja na mambo mengine watajifunza uzalendo, mbinu za kivita,utawala na usalama wa raia.
 Akizungumza katika mafunzo hayo Kasesela amesisitiza suala la usafi, kuacha ulevi, kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii na kuwa mwamminifu. Akimkaribisha Mkuu wa wilaya Kwa upande wake Mshauri wa Mgambo Mkoa wa Iringa Lt. Col. Kitta alisistiza kuwa wanao jifunza mgambo wana fursa nyingi sana za ajira hivyo wanatakiwa kujituma katika mafunzo ili mara  wamalizapo waweze kupa ajira
  Mpaka sasa katika wilaya ya Iringa mafunzo hayo yanafanyika katika Kata ya Wasa, Kihanga, Mboliboli na manispaa ya Iringa.
 




0 maoni:

Chapisha Maoni