Orodha
ya wachezaji 11 waliopo katika Kikosi Bora cha Mwaka cha Ligi Kuu ya
Uingereza kimetangazwa ambapo Vinara wa Ligi hiyo, Leicester City na
timu inayoshika nafasi ya pili, Tottenham wakiibuka vinara kwa kutoa
wachezaji wanne kila timu.
Wachezaji
wa Leicester City walioingia katika kikosi hicho ni Jamie Vardy, Riyad
Mahrez, N’Golo Kante na Wes Morgan huku Tottenham wakiwa na Harry Kane,
Dele Alli, Toby Alderweireld na Danny Rose.
Vilabu
vingine vilivyopata nafasi ya kuingiza wachezaji ni Manchester United
kupitia David De Gea, Arsenal kupitia Hector Bellerin na West Ham
kupitia Dimitri Payet.
0 maoni:
Chapisha Maoni