Jumatatu, 13 Juni 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA JESHI LA POLISI MWANZA


MSANGISACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
…………………………………………………………………………………………….
 WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA MADAWA YA KULEVYA AINA YA MIRUNGI WILAYANI NYAMAGANA.MTU MMOJA AMEJERUHIWA VIBAYA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA GARI NA PIKIPIKI WILAYANI ILEMELA.WATU WANNE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA POMBE AINA YA GONGO WILAYANI MISUNGWI
MNAMO TAREHE 12.06.2016 MAJIRA YA SAA 13:20HRS KATIAK NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO CHAKECHAKE KATA YA MKUYUNI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA KATIKA MISAKO WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WATATU AMBAO NI 1.TATU SALEHE MIAKA 41 MKAZI WA BUSWELU, 2. MARY PAULO MIAKA 21 MKAZI WA NYAKATO NA 3.MWANA RAMADHANI MIAKA 36 MKAZI WA SHEDE WAKIWA NA MIRUNGU KILO SITA {06} KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.
INADAIWA KUWA WATUHUMIWA PINDI WANAPOKUWA KATIKA NYUMBA HIYO YA WAGENI HUFANYA BIASHARA YA KUWAUZIA WATEJA WANAOFIKA MAHALI HAPO KUPATA HUDUMA YA VYUMBA, NA KUPELEKEA KUSHAMIRI KWA BIASHARA HIYO HARAMU YA MADAWA YA KULEVYA MAHALI HAPO.
AIDHA WATUHUMIWA WOTE WATATU WAPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI, ILI KUWEZA KUBAINI MTANDAO WA WATU WANAOSHIRIKIANA  KATIKA UTEKELEZAJI WA BIASHARA HIYO HARAMU MAHALI HAPO. UCHUNGUZI WA TUKIO HILO BADO UNAENDELEA PINDI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WOTE WATATU WATAFIKISHWA MAHAKAMANI KIJIBU MASHITAKA YANAYO WAKABILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA MARA MOJA TABIA YA KUJIHUSISHA NA BIASHARA ZA MADAWA YA KULEVYA AMBAYO YAMEKUA YAKIATHIRI VIJANA WENGI KATIKA JAMII ZETU, HIVYO JESHI LA POLISI LITAHAKIKISHA LINAWATAFUTA NA KUWAKAMATA WALE WOTE AMBAO WATAENDELEA NA BIASHARA HIYO YA MADAWA YA KULEVYA NA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI.
KATIKA TUKIO LA PILI

0 maoni:

Chapisha Maoni