Kampuni
ya KFC Kuku Foods Limited Tanzania leo imeanza rasmi kutoa mchango wa
vifaa vya braille kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kuona na kusikia wa
shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko iliyopo kariakoo. Kampuni ya KFC
imedhamiria kutoa msaada kwa shule hii yenye mahitaji maalum kwa kipindi
endelevu.
Katika
halfa ya makabidhiano ya vifaa maalum kwa Shule ya Msingi Uhuru
Mchanganyiko iliopo Kariakoo, KFC wamesema kuwa vifaa hivyo vitawasaidia
wanafunzi wenye mahitaji maalum ambao ni wasio na uwezo wa kuona na
wale wasioweza kusikia. Vile vile Msaada huo ni muundelezo wa
ushirikiano na uhusiano wa karibu kati ya Kampuni ya KFC na Shule ya
Msingi Uhuru Mchanganyiko.
Mwaka
jana KFC ilitoa mwaliko kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Uhuru
Mchanganyiko kuhudhuria ufunguzi maalum wa tawi lao lilipo Kariakoo
ambapo Shillingi Milioni Moja zilitolewa kwa ajili ya kusaidia shule
hiyo.
Meneja
Mkuu wa KFC Tanzania, Louis Venter amesema, “Dhumuni la Mchango wetu ni
kusaidia kuboresha mazingira ya kijamii ya watoto hawa. Tunataka
mchango huu wa kampuni yetu uwe wa maandalizi ya uzinduzi wa programu
maalum iitwayo ‘Add Hope Program’ ya kusaidia jamii nchini Tanzania
mwezi Oktoba mwaka huu.”
‘Add
Hope Program” ni mradi mahususi uliobuniwa na kampuni mama ya KFC na
unaoratibiwa duniani kote ambapo wateja wa KFC wanapata nafasi ya
kuchangia maendeleo ya jamii kwa kuongeza pesa kidogo kwenye malipo ya
gharama ya chakula walichoagiza.
Mradi
wa ‘Add Hope Program’ nchini Afrika ya Kusini ulianzishwa miaka sita
(06) iliyopita na umesaidia kupunguza na kutatua matatizo yanayowakumba
wananchi wa Afrika ya Kusini kama msaada kwa watoto katika masuala ya
lishe kuwasaidia watoto wapate lishe bora, kusoma na kustawi.
Nchini
Tanzania mapato yote ya Add Hope ikisha zinduliwa yataenda Shule ya
Msingi Uhuru Mchanganyiko , ikiwa ni pamoja na michango yote ya baadaye
yatakayotolewa na KFC.
Kwa
upande wa Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko, Mwalimu Mkuu Bibi Anna
Mshana ametoa shukrani za dhati kwa kampuni ya KFC kwa msaada wao wa
vifaa maalum kwa shule hiyo, “ Elimu ni hazina tosha kwa watoto wetu,
vifaa vilivyotelewa na KFC vitasaidia kuhakikisha kuwa wanafunzi wetu
wanasoma na kustawi katika mazingira yaliyo sahihi na tunafurahi kuwa na
rafiki wa karibu KFC,” alisema.
0 maoni:
Chapisha Maoni