Posted by Esta Malibiche on Sept29.2016 in BIASHARA
MENEJA Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti kushoto na Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso wakibadilishana mikataba
mara baada ya kuasini makubaliano ya uuzaji wa mafuta kwa kutumia kadi
ya Aiter Money Tap Tap , Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Mafuta
cha Puma Oysterbay.
MENEJA Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti kushoto na Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso wakiasini mkataba wa
makubaliano ya uuzaji wa mafuta kwa kutumia kadi ya Aiter Money Tap Tap ,
Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Mafuta cha Puma Oysterbay jijini
Dar es salaam.
Baadhi ya maofisa wa Puma na
Aiter wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye kituo cha mafuta cha
Puma Oysterbay jijini Dar es salaam.
Meneja Rasilimali Watu wa Puma
Tanzania Bi Loveness Hoyange pamoja na maofisa wengine wa kampuni hiyo
na kampuni ya Kampuni ya simu ya Aitel wakifuatilia matukio katika hafla
hiyo.
Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matindekulia na baadhi ya maofisa wa kampuni ya Aitel na Puma wakifuatilia matukio katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso kulia na
MENEJA Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti wakishuhudia
wakati mmoja wa wateja wa Aitel Money na Puma akijaziwa mafuta kwa
kutumia huduma ya Airtel Money Tap Tap katika kituo cha mafuta cha Puma
Oysterbay jijini Dar es salaam.
…………………………………………………………………………………..
MENEJA Mkuu wa Puma Energy
Tanzania Philippe Corsaletti amesema wanalo jukumu la kuhakikisha
huduma wanazitoa kwa ajili ya Watanzania zinakuwa salama wakati wote
ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za
kuhamasisha kutumia njia za kieletroniki kwenye malipo ya fedha.
Corsaletti alitoa kauli hiyo
Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa huduma mpya inayojulikana kwa
jina la Airtel Money Tap Tap ambayo inamuwezesha mteja wao anapotaka
kununua mafuta kwa kutumia kadi ya Airtel badala ya kutoa fedha taslimu
akiwa kituo cha mafuta.
Alisema wanahisi kwamba
wanawajibu wa kufanya huduma zao kwa usalama, senye ufanisi na rahisi
zaidi kwa wateja wao na kufafanua ni hatari kubeba fedha wakati wote
maana ni rahisi kuhatarisha maisha.
Aliongeza hivyo ili kufanya
jamii ya Watanzania inakuwa salama wakati wote imeona kuna haja ya kuwa
na huduma hiyo ambayo itamuwezesha anayehitaji kununua mafuta kwenye
vituo vya Puma vilivyopo maeneo mbalimbali ya Dar es salaam wanatumia
kadi za Airtel kununua mafuta.
“Milango yetu iko wazi kwa
ajili ya kuendelea kuboresha huduma zetu na kuna jambo lolote ambalo
tunaweza kulifanya ili jamii yetu kuwa salama wakati wote.Hivyo kuna
umuhimu wa kuwa na matumizi ya kadi ya Airtel katika kununua mafuta
kwenye vituo vyetu vya Puma,”alisema.
Akifafanua zaidi kuhusu huduma
ya Airtel Money Tap Tap, Corsaletti alisema chini ya utaratibu huo mtu
yeyote aliyejisajili na huduma ya Airtel Money atakuwa na uwezo wa
kulipia bidhaa za Puma katika vituo vyake vyote nchini kwa kutumia kadi
ya huduma ya Airtel Tap Tap badala ya kutumia fedha kwa ajili ya
huduma kama hizo.
“Kadi hii imeundwa kwa namna
ambayo wakati wa kutumika kufanya malipo , hupunguza fedha kwa kiasi
cha malipo kutoka katika akaunti ya Airtel Money ya mnunuzi kwenda
kwenye akaunti ya muuzaji. “Kadi hii itakuwa inauzwa kwa bei ya Sh 2,
000 kwenye vituo vyote vya Puma Dar es Salaam na maduka yote ya Airtel
Tanzania .
Kuanzia mwakani kadi hii itakuwa pia inapatikana katika vituo vyote vya mikoani ambavyo vipo chini ya Puma,”alisema.
Alitumia nafasi hiyo kueleza
kuwa Puma Tanzania ina jumla ya vituo 46 nchini kote na kwa kuanza,
vituo vyote vya Dar es Salaam vitakua vinatoa huduma hiyo, hali vituo
vingine vilivyosalia vitaunganishwa hivi kuanzia mapema mwakani.
“Lengo letu ni kuhakikisha
kwamba aina yoyote ya biashara tunayofanya, inafanyika kwa namna ambayo
mtumiaji wa mwisho anaridhika, na kubaki salama.
“Tunaamini hili kuwa jukumu
letu kwa jamii popote wanapotumia huduma zetu. Kwa kutumia kadi hii ya
Airtel Money Tap Tap, mtu hatahitaji kubeba tena hela tasilimu ili
kupata huduma katika kituo cha Puma,”alisisitiza.
0 maoni:
Chapisha Maoni