Jumatano, 14 Septemba 2016

GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA PROFESA BENNO NDULU ASEMA HALI YA UCHUMI WA TANZANIA NI IMARA, ASEMA “WAPIGA DILI” WAMEDHIBITIWA

5r5a1909


Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu, akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Museum wa Benki hiyo jijini Dar es Salaam, leo Septemba 14, 2016 kuhusu hali ya uchumi wa taifa. (PICHA NA K-VIS BLOG/Khalfan Said)
Profesa Ndulu na wasaidizi wake kutoka kushoto, Meneja Uhusiano na masuala ya peotokali, Zaria K. Mbeo, Mkurugenzi wa Sera na Uchumi, Johnson Nyela, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mabenki, Kened A. Nyoni, wakinakili maswali toka kwa waandishi wa habari
 Profesa Ndulu akizungumza
Bibi Mbeo
 
Taarifa ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu kwa Waandishi wa habari hii hapa chini
……………………………………………………………………………
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu, amesema hali ya uchumi wa
Tanzania ni ya kuridhisha tofauti na taarifa zinazozagaa kuwa uchumi wa nchi umedorora.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Museum wa Benki hiyo jijini Dar es Salaam, leo Septemba 14, 2016, Gavana huyo alisema, hali ya uchumi ni imara kwa vile tangu kuingia kwa serikali ya awamu ya Tano,
mfumuko wa bei umedhibitiwa na unashuka siku hadi siku hali kadhalika, thamani ya shilingi nayo inaendelea kuimarika.
Profesa Ndulu pia alisema,si kweli kwamba, fedha zimepungua mitaani bali fedha zipo ila fedha za “dili”ni kweli “zimekauka” na hii ni kutokana na jitihada za serikali katika kuziba mianya ya rushwa, wakwepa kodi na matumizi mabaya fedha za umma.
Aliwatoa hofu wananchi kwa kusema kuwa, hali ya uchumi wetu itaendelea kuimarika katika mwaka 2016 kutokana na viashiria kadhaa ambavyo ni pamoja na uzalishaji wa umeme katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016, umeongezeka kwa asilimia 14.5 kufikia KwH milioni  3,454.2 ikilinganishwa na na kWh milioni 3,016.7 katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
Akifafanua zaidi alisema, ongezeko hilo la umeme limetokana na jitihada za serikali katika kutumia nishati ya gesi kwenye uzalishaji umeme kufuatia kukamilika kwa bomba la gesi kutoka Mtwara na Lindi hadi Dar es Salaam pamoja na mtambo wa Kinyerezi I. “Umeme unaozalishwa kwa kutumia nishati ya gesi umeongezeka kwa asilimia
52.2, hali itakayosaidia kuongezeka kwa uzalishaji viwandani pamoja na sekta nyingine zinazotegemea nishati ya umeme, na hivyo kuchangia katika kuongeza pato la Taifa na pia ghjarama ya umeme itashuka.” Alisema.
“Kumekuwepo na taarifa nyingi zinazozagaa kuwa uchumi umedorora, lakinikwanza napenda niweke wazi, mimi si mwanasiasa, mimi nataka kulizungumzia swala hili kitaalamu, ukiangaliatakwimu za Ofisi ya Takwimu ya Taifa, hali ya ukuajiwa uchumi wa Tanzania imeendelea kuwa ya kuridhisha, katika robo ya kwanza ya mwaka 2016, ukuaji wa Pato la Taifa unakadiriwa kuongezeka  kwa asilimia 5.5 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 5.7 katika kipindi kama hicho mwaka 2015, sasa kwa takwimu hizi hauwezi kusema uchumi umedorora, hii si kwelikabisa,” alisema Profesa Ndulu.
Taarifa kamiliya Profesa Benno Ndulu kuhusu hali ya uchumi soma hapo chini.

0 maoni:

Chapisha Maoni