Miradi ya maendeleo 15 yenye thamani ya shilingi bilioni 8,391,131,054 imetembelewa na mwenge wa uhuru katika halmashauri za manispaa na singida wilayani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias
Tarimo amesema miradi hiyo imejikita katika sekta za afya, maji, elimu,
barabara, kilimo, ufugaji, miradi ya akina mama na vijana pamoja na
vilabu vya wapinga rushwa na madawa ya kulevya.
Tarimo amesema katika halmashauri
ya manispaa miradi iliyowekewa mawe ya msingi ni pamoja na stendi mpya
ya mabasi yaendayo mikoani ambapo mradi huo una thamani ya shilingi
bilioni 3,726,072,678 na mradi wa barabara ya kiwango cha lami wenye
thamani ya bilioni 2,694,339,096.
Aidha katika upande wa kuwajengea
uwezo vijana kiuchumi manispaa imeendelea kutenga asilimia kumi ya
bajeti ya mwaka ili kuwawezesha vijana mafunzo ya namna ya kubuni miradi
na kuiendeleza.
Katika mapambano dhidi ya Ukimwi
Tarimo amesema manispaa imeweza kuanzisha vituo kumi vya kupima Ukimwi
na kutoa ushauri nasaha, vituo 26 vya kuzuia maambukizi kutoka kwa mama
kwenda kwa motto na vine vya kutoa dawa za kufubaza VVU.
Amesema kwa kipindi cha Januari
2015 mpaka septemba 2016 wakazi wa manispaa 19,591 wamepima VVU ambapo
waliopatikana na maambukizi ya VVU ni 1,124.
Kwa upande wa ugonjwa wa maralia
ambapo kauli mbiu yake ni “wekeza katika maisha ya baadaye tokomeza
maralia” manispaa imefanikiwa kupunguza maambukizi na vifo vitokanavyo
na ugonjwa huo kutoka asilimia kumi mwaka 2014 hadi asilimia 3.7 mwaka
2015 kutokana na juhudi za manispaa za kutoa elimu ya kuteketeza mazalia
ya mbu na matumizi ya vyandarua vilivyowekewa da ya viuatilifu.
Tarimo amefafanua kuwa wananchi
wanaelimishwa na kushauriwa kuwahi hospitali pindi wanapoona dalili za
homa na si kujinywea dawa bila maelekezo ya wataalamukwani si kila homa
ni malaria na endapo watagundulika kuwa na ugonjwa wa malaria
wanashauriwa kutumia dawa mseto na kukamilisha dozi.
Kwa upande wa halmashauri ya
singida, mwenge wa uhuru umezindua na kuweka mawe ya msingi katika
miradi minane yenye thamani ya milioni 989,039,279 ambapo nguvu ya
wananchi ni shilingi milioni 84,186,600, halmashauri ya wilaya ni
milioni 21,607,450, wahisani ni 76,742,000 na serikali kuu
806,503,229 pamoja na kuhamasisha wananchi juu ya umoja, mshikamano na
uzalendo.
Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa
maji wa kijiji cha Itaja wenye thamani ya shilingi milioni 411,405,887
uliokamilika mwezi Mei pamoja na miundombinu ya nyumba ya mashine,
ufungaji wa jenereta na pamu za kusukumia maji, ujenzi wa njia kuu ya
kupeleka maji kwenye matanki na ujenzi wa mtandao wa kusambaza maji
kwenye vituo vya kuchotea maji.
Mradi huo utakaonufaisha wakazi
wa Itaja kwa kuwapatia maji safi na salama umekabidhiwa kwa jumuiya ya
watumia maji iliyopewa mafunzo ya uendeshaji na iko chini ya uangalizi
kwa kipindi cha miezi sita.
Naye Kiongozi wa mbio za mwenge
wa uhuru George Jackson Mbijima ameweka jiwe la msingi ujenzi wa kiwanda
cha kusindika mbogamboga kijiji cha msange na kuwashauri wanakikundi
kuendeleza usindikaji wa mazao hayo kwani ni changamoto kwa wakulima
kutokana na kuharibika haraka.
Amesema mradi ukisimamiwa utakuwa
mkombozi wa wakulima kutokana na kuwa wakulima wengi hulalamika
kuharibika mazao kutokana na kukosa masoko haraka hasa kwa mazoa ya
mbogamboga, aidha mradi utatengeneza ajira kwa vijana na akina mama
wengi wa kijiji cha msange na halmashauri ya Singida.
Ameongeza kwa kusisitiza kuwa
mradi utaboresha afya ya wanajamii wanaouzunguka na kuwashukuru wahisani
waliotoa shilingi milioni 47,000,000, huku halmashauri ikichangia
milioni 2,000,000 na wananchi milioni 4,046,000 katika kufanikisha
ujenzi wa kiwanda hicho.
Miradi mingine iliyotembelewa na
mwenge wa uhuru halmashauri ya Singida ni pamoja na klabu ya wapinga
rushwa shule ya sekondari Mughamo, mradi wa vijana wa ufugaji nyuki na
uhifadhi wa mazingira kijiji cha Msikii, Mradi wa utunzaji wa mazingira
sekondari ya Mrama, ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Mwahango na ujenzi
wa ghala la kuhifadhia alizeti Kata
0 maoni:
Chapisha Maoni