Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema limewakamata zaidi ya
watu 20 ambao kati yao wanahusishwa na tukio la mauaji ya askari polisi
4 lililotokea siku za hivi karibuni maeneo ya Mbande, jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Kanda hiyo
Kamanda Simon Sirro amesema kuwa watu hao wamekamatwa katika operesheni
inayoendelea kufanywa na jeshi hilo maeneo ya Vikindu nje kidogo ya
jiji la Dar es Salaam.
“Operesheni
inapata mafanikio makubwa tangu ilipoanza na kwamba tumewakamata watu
zaidi ya 20 maeneo ya vikindu na Dar es Salaam wakihusishwa na matukio
mbalimbali ikiwemo lile la mauaji, ” amesema.
Aidha,
Kamanda Sirro amewashukuru viongozi wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) kwa kuaghirisha operesheni Ukuta waliyoipanga
kuifanya kesho.
“Niwapongeze
kwa maamuzi ya busara waliyofanya maana ni ya kizalendo, niwahakikishie
tu kwamba Dar es Salaam iko salama na pia niwatoe hofu wananchi kuwa
wasiogope watakapo waona askari barabarani sababu kazi yao ni kufanya
doria ili jiji liwe salama, ” amesema.
Pia
amesema Viongozi waandamizi wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama
hicho taifa Freeman Mbowe na Edward Lowassa waliotakiwa kuripoti kesho
Katika kituo hicho, wanatakiwa kuripoti siku ya jumanne ya wiki
ijayo.Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema
limewakamata zaidi ya watu 20 ambao kati yao wanahusishwa na tukio la
mauaji ya askari polisi 4 lililotokea siku za hivi karibuni maeneo ya
Mbande, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Kanda hiyo
Kamanda Simon Sirro amesema kuwa watu hao wamekamatwa katika operesheni
inayoendelea kufanywa na jeshi hilo maeneo ya Vikindu nje kidogo ya
jiji la Dar es Salaam.
“Operesheni
inapata mafanikio makubwa tangu ilipoanza na kwamba tumewakamata watu
zaidi ya 20 maeneo ya vikindu na Dar es Salaam wakihusishwa na matukio
mbalimbali ikiwemo lile la mauaji, ” amesema.
Aidha,
Kamanda Sirro amewashukuru viongozi wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) kwa kuaghirisha operesheni Ukuta waliyoipanga
kuifanya kesho.
“Niwapongeze
kwa maamuzi ya busara waliyofanya maana ni ya kizalendo, niwahakikishie
tu kwamba Dar es Salaam iko salama na pia niwatoe hofu wananchi kuwa
wasiogope watakapo waona askari barabarani sababu kazi yao ni kufanya
doria ili jiji liwe salama, ” amesema.
Pia
amesema Viongozi waandamizi wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama
hicho taifa Freeman Mbowe na Edward Lowassa waliotakiwa kuripoti kesho
Katika kituo hicho, wanatakiwa kuripoti siku ya jumanne ya wiki ijayo.
0 maoni:
Chapisha Maoni