Posted by Esta Malibiche on Sept29.2016
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw.
Deodatus Kinawiro akiongea na Baraza la Madiwani la halmashauri ya
bukoba na kuwataka kuacha kulalamika hasa katika kipindi hichi cha
kurudisha hali ya kawaida baada ya tetemeko la ardhi kutokea bali
watafute njia itakayoleta majawabu ya mambo yanayojitokeza.
Baadhi ya Madiwani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro wakati wa kikao cha dharura cha baraza hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw.
Deodatus Kinawiro akiongea na wanafunzi wa shule ya msingi Kashai
iliyoripotiwa na moja ya kituo cha televisheni nchini kuwa shule hiyo
imefungwa kutokana na athari za tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw.
Deodatus Kinawiro akiongea na walimu wa shule ya msingi Kashai
alipowatembelea ili kuona maendeleo ya wanafunzi baada ya taarifa za
upotoshaji zilizotolewa na moja ya kituo cha televisheni nchini kuwa
shule hiyo imefungwa kutokana na athari za tetemeko la ardhi mkoani
Kagera.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw.
Deodatus Kinawiro akikagua nyumba za muda za walimu wa shule ya msingi
Kaishaza mkoani Kagera baada ya nyumba zao kuathirika na tetemeko la
ardhi mkoani Kagera.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro akikagua ujenzi wa miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera. |
0 maoni:
Chapisha Maoni