Posted by Esta Malibiche on Sept 26.2016 in BIASHARA
TUPO TAYARI KUJA KUWEKEZA KATIKA NCHI YA TANZANIA NA HUSUSAN KATIKA MKOA WA MWANZA, NDIVYO ANAVYO ONEKANA KUSEMA SON YOUNG SOO, KIONGOZI WA MSAFARA KWA MKUU WA MKOA WA MWANZA.
MKUU WA MKOA WA MWANZA JOHN
MONGELLA AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAJUMBE WA MKUTANO HUO MARA
BAADA YAKUFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE KUTOKA NCHINI KOREA KUSINI.
MKUU WA MKOA WA MWANZA JOHN MONGELLA AKIMUELEKEZA JAMBO MKURUGENZI WA MANISPAA YA ILEMELA JUU UJUMBE KUTOKA KOREA KUSINI.
FURSA NI JAMBO MOJA UTAYARI WA
WANANCHI WETU NI JAMBO JINGINE, NIWAOMBE WANANCHI KWA UJUMLA WAO WAWE
TAYARI KUSHIKIANA NA WAWEKEZAJI. NAIBU WAZIRI WA ARDHI NA MBUNGE WA
ILEMELA, DKT. ANGELINA MABULA.
TUNAPOSEMA, MWANZA KAZI NA
MAENDELEO NDIO HII TAFSIRI YAKE, KOREA KUSINI WAMEKUJA, KWASABABU YA
AMANI NA UTULIVU WA NCHI YETU, RC MONGELLA (PICHA ZOTE NA OFISI YA RC
MWANZA),
………………………………………………….
- Awaahidi ushirikiano.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John
Mongella, amepokea ujumbe wa wawekezaji kutoka nchini Korea Kusini,
wenye niya yakuwekeza katika mkoa wa Mwanza ukiwa na ujumbe wa watu kumi
na watano nakufanya nao mazungumzo mapema katika Ofisi yake kabla
yakuendelea na ziara yao katika Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.
Katika mazungumzo yao yaliyodumu
saa 1:33, Mkuu wa Mkoa amewahakikishia utayari wa mkoa wa Mwanza
kuwapokea wawekezaji kutoka nchini humo lakini pia kuwabainishia maeneo
mbali mbali katika sekta ya uchumi ambayo watu wa Korea kusini wanaweza
kuwekeza.
Alianza kwakuwashukuru sana
kwakutambua urafiki wa nchi hizi mbili ambao umeanza miaka ya 1960’s, na
kuwaambia kuwa Mwanza ni mkoa ambao una fursa nyingi za uwekezaji
katika Nyanja mbali mbali ikiwapo: Viwanda, Biashara, Kilimo, uvuvi,
Mifugo, kwakutaja baadhi.
Mkuu huyo wa mkoa ameuwambia
ujumbe huo wa watu wa jamhuri ya Korea kusini, uliokuwa unaomngozwa na
Bw. Son Yang Soo, kuwa Mwanza ndio sehemu pekeee katika nchi za eneo la
maziwa makuu inayo liunganisha soko la Afrika Mashariki kwa nchi za
South Sudan, Rwanda, Burudi, Jamhuri ya Congo na hata Kenya na Uganda
Mkuu wa mkoa amesema kutoka na
uchumi wa Mkoa wa Mwanza kufikia Tril. 8.45 kwa mwaka katika uzalishaji
lakini pia Mwanza ndio mkoa unaochangia pato la Taifa ukishika nafasi ya
pili ambapo mchango wake ni asilimia 9.4 katika pato la taifa
ukitanguliwa na Dar es Salaam unaochangia kwa asilimia 17 kwa mwaka,
hivyo kwa watu wanaotaka kuwekeza Mwanza wamewaza vyema kama jinsi
ujumbe huu wa Korea Kusini ulivyo fanya.
Naye kiongozi wa msafara huo,
Song Young Soo, alianza kwakuwapa Watanzania pole kufuatia tetemeko la
Ardhi lililotokea tarehe 10, Septemba na kuathiri zaidi Mkoa wa Kagera
na mara baada ya hapo, akasema wamefurahishwa na jitihada zinazo
chukuliwa na mamlaka ya serikali katika kuahakikisha wawekezaji wanapata
fursa yakuwekeza, Song amesema katika Nchi ya Korea Kusini uwekezaji
umejikita katika nyanja za Teknolojia ya habari na mawasiliano, Afya na
Viwanda kwa ujumla, aidha amesema kufuatia ziara iliyofanywa na mbunge
wa Ilemela na Ujumbe wake mapema Mwaka huu, hiyo sasa imeibua chachu na
muendelezo wa ushirikiano wanachi wan chi hizi mbili ambazo zimekuwa na
ushirikiano wa muda mrefu sasa.
Kwa Upande wake Naibu Waziri wa
Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makaazi Dkt. Angeline Mabula (MB),
amewataka wana watanzania na wana Mwanza kwa ujumla wao , kuonesha
utayari na kuwapokea wageni wanao kuja kwa nia njema yakuwekeza katika
Mkoa wa Mwanza “ Niwa ombe tuu wananchi wa Tanzania, kuonesha utayari
wakupokea wawekezaji, tunaimba viwanda, viwanda vikiwapo watakao ajiriwa
ni watanzania wenye sifa husika, hivyo nilazima tunapopata wawekezaji
tuwe na utayari na ukarimu kwa wageni wetu hasa wawekezaji wema na
kuwapa ushirikiano kwenye maeneo yetu,” alisema Mabula.
Ujumbe huo wa Korea Kusini
ulikuwa ukiongozwa na Song Yaung Soo, wajumbe wengine ni Shing Jong Sam,
Cho Yoop Gon, Kim Gi Geob, Doewak Kim, KTM Kyu il, wengine ni Rark in
Nwan, Kim Il Hyun, Kim Ji Mi, Lee Suk Hoom, Kim Chan Kyu, Byun Kyumg
Ho, Lee Joom Hwa na Kim Lim Gon na Mkalimani wao aliyekuwa anaitwa Alex
Gang.
Ujumbe huo wa Korea pamoja na
mambo mengine utatembelea eneo la Nyamongholo kisha utapata fursa
yakujionea Matayarisho ya Mpango Kamambe ya urasimishaji wa Makaazi ya
Jiji la Mwanza na mpangilio wake.
Imeandaliwa na Afisa habari na Uhusiano Mwanza
0 maoni:
Chapisha Maoni