Posted by Esta Malibiche on Sept14.2016 in News
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
na Mbunge wa Iramba Magharibi Mhe. Mwigulu Nchemba akipata maelezo
kutoka kwa Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati NIDA;
Bi. Rose Mdami mara baada ya kupokea kitambulisho chake cha Taifa.
Mbunge wa Igunga Dkt. Dalaly Peter
Kafumu akiwa amejawa na furaha baada ya kupokea Kitambulisho chake
kipya chenye saini Kinachotolewa na NIDA katika zoezi la ugawaji wa
vitambulisho hivyo kwa waheshimiwa Wabunge, Bungeni Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
na Mbunge wa Iramba Magharibi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba; akiweka saini
katika orodha ya majina ya wabunge baada ya kupokea Kitambulisho chake
kipya chenye saini Bungeni Dodoma. Kushoto ni Afisa wa Mifumo ya
Kompyuta NIDA Bi. Zainabu Mavere.
Mhe. Azzan Mussa Zungu Mbunge wa
Jimbo la Ilala (wapili kulia) mara baada ya kuchukua kitambulisho chake
chenye saini Bungeni Dodoma. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano na Hifadhi Hati Bi. Rose Mdami, kushoto ni Afisa Usajili
NIDA Bw. Thadei Minja na wa pili kushoto ni Afisi Usajili wa Wilaya ya
Dodoma Mjini Bwana Khalid Mrisho.
Mbunge wa Singida Magharibi Mh.
Elibariki Emmanuel Kingu akiwa mwenye furaha baada ya kuchukua
Kitambulisho chake chenye saini leo bungeni Dodoma, ambapo NIDA imeanza
kugawa vitambulisho vyenye saini kwa waheshimiwa Wabunge. Kushoto ni
Afisa Usijili Wilaya ya Dodoma Mjini Bw. Khalid Mrisho.
Mh. Seif Khamis Said Gulamali
Mbunge wa Jimbo la Manonga kwa furaha akionyesha kitambulisho chake
kipya chenye saini baada ya kupokea kutoka kwa Afisa Usajili wa NIDA
wilayani Dodoma Mjini Bwana Khalid Mrisho Bungeni Dodoma.
Afisa wa Jeshi la Polisi,
akithibitisha kupokea kitambulisho chake kwa kuweka saini kwenye daftari
maalumu la kumbukumbu, baada ya kuchukua Kitambulisho chake leo bungeni
Dodoma. Zoezi la ugawaji wa Vitambulisho vyenye saini limeanza katika
ofisi za
……………………………………………………
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania leo wamekuwa miongoni mwa wananchi walioanza
kuchukua Vitambulisho vipya vya Taifa vyenye saini; kufuatia utaratibu
uliotangazwa hivi karibuni na Nida wa kuanza kugawa vitambulisho vipya
kwa makundi mbalimbali waliokamilisha taratibu za usajili
Shughuli ya kugawa
Vitambulisho vya Taifa kwa Waheshimiwa Wabunge imeanza rasmi leo
bungeni; pamoja na kuendelea kuwasajili wabunge ambao kwa sababu moja au
nyingine hawakusajiliwa wakati wa zoezi la awali la usajili
Mbali na waheshimiwa
Wabunge; wengine ni wafanyakazi wa Bunge na watumishi katika taasisi na
Wizara mbalimbali ambao walisajiliwa katika utaratibu wa kawaida wa
Usajili. Zaidi ya waheshimiwa Wabunge 240 wanakusudiwa kupatiwa
vitambulisho vyao.
0 maoni:
Chapisha Maoni