Jumanne, 27 Septemba 2016

WAZIRI LUKUVI AWAFUTIA HATI WALIOMIKISHWA ENEO LOTE LA MAKABURI YA KINYEREZI SOKONI

Poested by Esta Malibiche on Sept27.2016 in  NEWS



bn647561
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, William Lukuvi akisalimia na DAS wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, alipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni, kufuatia mgogoro wa wananchi wawili kumilishwa eneo hilo la makaburi lenye ukubwa wa zaidi ya ekari moja. Katika sakata hilo, Waziri Lukuvi ameagiza kufutwa kwa umiliki huo mara moja ifikapo leo jioni, na pia kugiza kusakwa Pascal Kyonya Kazungu na  Ntitonda Chukilizo waliomilikishwa eneo hilo watafutwe na kufikishwa ofisini kwake kesho  Kadhalika amemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Ardhi mkoa wa Dar es Salaam, Leo Komba, kuorodhesha majina ya maofisa ardhi wote walioshiriki kuwamilikisha ardhi hiyo ya eneo la makaburi ili aweze kuwashughulikia kwa kuwachukulia hatua za kisheria. Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Segerea Bona Kalua
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi William Lukuvi akipatiwa maelezo na Mbunge wa Segerea Bona Kalua alipowasili kwenye eneo hilo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni leo. Kushoto ni DAS wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo.
 Waziri Lukuvi akiwa na Diwani wa Kata ya Kinyerezi,  Grayson Celestine alipowasili leo kutatua mgogoro wa kumilikishwa eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni Dar es Salaam,.Kushoto ni Dar wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo
 Waziri Lukuvi akihoji jambo kwa uongozi wa Kata ya Kinyerezi alipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni, leo
 Waziri Lukuvi akipata maelezo kutoka kwa uongozi wa Kata ya Kinyerezi alipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni, leo. Kulia ni Mbunge wa Segerea Bona Kalua
 Wananchi wa eneo la Kinyerezi Sokoni wakiwa wamemzunguka Waziri Lukuvi alipowasili kwenye eneo la Makaburi hayo leo
 Kaimu Mkurugenzi wa Ardhi jiji la Dar es Salaam,  Leo Komba (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri Lukuvi kuhusu anachofahamu juu ya wananchi wawili kumilikishwa eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni leo
 ” Sasa hapo mimi sima la ziada, Wewe si ndiyo Mkurgenzi?” Sawa kuanzia mda huu, nakuagiza ukafute umilikishwaji ardhi uliofanywa katika eneo la makaburi haya”, alisema Waziri Lukuvi na kuongeza ” Na wale waliomilikishwa hapa nitafutieni kesho waje kwangu wanieleze ilikuwaje hata wakapata kumilikishwa eneo hili, na wale wote walioshiriki kwa namna yoyote katika kufanya hili uniletee majina yao mara moja”.
 Diwani wa Kata ya Kinyerezi, Grayson Celestine, akimshukuru Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi, William Lukuvi baada ya kutoa uamuzi wa kufuta umilikishwaji wa eneo hilo la makaburi kwa watu wawili. 
Waziri Lukuvi akifuatana na DAS wa wilaya ya Ilala wakati akiondoka kwenye eneo hilo la makaburi ya Kinyerezi, ambako amefanikiwa kumaliza mgogoro wa wananchi na watu wawili waliokuwa wamemikishwa eneo hilo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni. Kulia ni Diwani wa Kata ya Kinyerezi Grayson Celestine. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
………………………………………………………….
Jonas Kamaleki, MAELEZO
Wakazi wa Kinyerezi Sokoni, Dar es Salaam wameipongeza Serikali ya awamu ya Tano kwa kufuta hati tatu zilizokuwazimetolewa katika eneo la makaburi liliouzwa kinyume cha sheria.
Pongezi hizo zimetolewa leo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi baada ya kumwagiza kamishna wa ardhi Kanda ya Dar es Salaam kufuta hati hizo mara moja na kulirejesha eneo la makaburi kwa wananchi.
Akiongea kwa niaba ya wakazi wa Kinyerezi, Mwanasheria, Mwinjuma Mzee amesema kuwa Wanakinyerezi wanamshukuru sana Mhe. Waziri kwa kurejesha eneo la makaburi kwa wakazi hao.
“Mhe. Waziri na msafara wake wote tunawashukuru kwa kumaliza mgogogoro huu ambao umedumu kwa muda mrefu na tumemwomba Waziri ashughulikie na maeneo mengine yanayohusu huduma za jamii kama zahanati na shule,” alisema Mzee.
Naye mkazi wa Kinyerezi, Bi. Maimuna Forogo ameelezea furaha yake kwa kumshukuru sana Mhe waziri kwa hatua aliyoichukua ya kubatilisha hati za umiliki wa makaburi.
“Mimi namnshukuru sana Mhe. Waziri na Serikali ya awamu ya Tano kwa ujumla kwa kutujali sisi wananchi, mimi kwenye makaburi haya nilimzika babu yangu sasa wanataka nimpeleke wapi kwanza ni mifupa mitupu,”alisema Maimuna.
Kwa upande wake, Mhe. Lukuvi amesema ameamua kubatilisha hati tatu za viwanja zilizotolewa na watumishi wasiowaaminifu wa Serikali ili eneo hilo liendelee kutumika kwa ajili ya maziko.
“Nimemuagiza kamishna anitafutie wahusika ambao walishiriki katika kumilikisha eneo la makaburi kwa watu ili wachukuliwe hatua za kinidhamu, watu hawa inabidi wafukuzwe kazi kwani kitendo cha kumilikisha eneo la kuzika hakivumiliki,”alisema Waziri Lukuvi.
Ameongeza kuwa watu ambao wanadiriki kuuza makaburi ambayo yametumiwa tangu mwaka 1962 na kwa sasa yapo zaidi ya 500, ni watu ambao hawana hata hofu ya Mungu hivyo kufukuzwa ni halali yao.
Mhe. Lukuvi ametoa wito kwa viongozi wenzake wanapofanya shughuli za mipangomiji nchini kutenga sehemu za huduma za jamii ikiwemo mahali pa kuzikia kwani kila mtu atakufa na anahitaji kuzikwa.  
“Serikali ya awamu ya Tano tumeamua kurekebisha pote palipokuwa pamepinda ili wananchi wapate haki zao,”alisema Lukuvi.
Aidha amewataka waliokuwa wamemilikishwa wafike wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili wampe Waziri uzoefu wanaoutumia kununua maeneo ya huduma za jamii ikiwemo maeneo ya makaburi ili imsaidie kujua jinsi mtandao ulivyo.
Hati tatu zilizofutwa ni 213, 215 na 217 Kitalu B, Kinyereze, Kata ya Segera jijini Dar es Salaam.

0 maoni:

Chapisha Maoni