Mchezaji wa Timu ya Serengeti Boys
Mohamed Rashid Abdalla akikokota mpira mbele ya wachezaji wa timu ya
taifa ya Congo Brazaville katika mchezo wa kuwani kufuzu fainali za
Mataifa ya Afrika kwa vijana liofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini
Dar es salaam, mpira umekwisha timu ya Serengeti Boys imeshinda magoli
3-1 dhidi ya Congo Brazaville yaliyofungwa na mchezaji Yohana Mkomola
katika dakika za 40 na 42. goli la tatu la Serengeti Boys limefungwa na
Issa Makamba aliyeingia kipindi cha pili huku Congo Brazaville wakipata
magoli mawili.
Mchezaji wa timu ya Serengeti Boys
Israel Mwenda akiruka juu juu na mchezaji wa Congo Brazaville Moundza
Prince wakati mchezo huo ukiendelea kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys.
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Congo Brazaville
Viongozi mbalimbali wakiwa katika jukwaa kuu wakiimba wimbo wa Taifa.
Timu zote zikiingia uwanjani tayari kwa kuza kwa mpambano huo.
Waamuzi wa mchezo huo wakiongoza vikosi vya Timu ya Serengeti Boys na Congo Brazaville kuingia uwanjani tayari kwa mchezo huo.
Kikundi cha ushangiliaji cha timu ya taifa ya vijana Serengeti Boys.
Mashabiki wakishangilia kwa nguvu mara baada ya Serengeti Boys kupata magoli katika kipindi cha kwanza.
0 maoni:
Chapisha Maoni