Posted by Esta Malibiche on Sept27.2016 in NEWS
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim
Majaliwa akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya, Bernard Konga alipotembelea banda la upimaji afya katika
Uwanja wa Taifa wakati wa Mechi ya Wabunge wa Simba na Yanga.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mfuko huo.
Waziri wa Habari Bw. Nape Nnauye
akiongozana na Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma wa NHIF, Bi. Grace Michael
kuelekea kwenye banda la Mfuko huo ambalo liliendesha upimaji wa afya
kwa wananchi wote waliofika uwanjani hapo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,
Bernard Konga akipokea cheti kutoka kwa Waziri Mkuu ambacho kinautambua
mchango wa Mfuko katika janga la tetemeko lililotokea mkoani Kagera.
Mbunge wa Sengerema Bw. William Ngeleja akipima uzito kabla ya mtanange kati ya wabunge wa Yanga na Simba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Gabriel akipima kiwango cha
sukari katika banda la NHIF.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Nape Nnauye akipima uzito kabla ya mechi kuanza.
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim
Majaliwa akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya, Bernard Konga alipotembelea banda la upimaji afya katika
Uwanja wa Taifa wakati wa Mechi ya Wabunge wa Simba na Yanga.
…………………………………………………………..
Na Grace Michael
WAZIRI Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim
Majaliwa ameupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima kwa kazi kubwa inayofanya ya
kuwahudumiwa wanachama wake lakini pia kuendesha shughuli za upimaji wa
afya bure katika maeneo mbalimbali.
Pamoja na pongezi hizo, ameutaka
Mfuko huo kuangalia namna ya kuwafikia Watanzania wengi zaidi katika
suala la upimaji wa afya ili kila mmoja ajue hali ya afya yake.
“Kwanza niwapongeze tu kwa kazi
kubwa mnayoifanya hapa ya kutupima afya zetu…hakikisheni shughuli hizi
zinafanyika mahali pengi zaidi kwani kwa sasa kuna mwamko mkubwa sana wa
wananchi kupima afya zao, hata pale bungeni leteni huduma hizi wakati
wa bunge ili waheshimiwa wabunge nao wapate fursa hii,” alisema Waziri
Mkuu.
Alisema kuwa Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya umekuwa msaada mkubwa katika usimamizi na utoaji wa huduma
za matibabu kwa wanachama wake pamoja na uboreshaji wa huduma za
matibabu.
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo
kutoa wito kwa wananchi kujiunga na huduma za Mfuko ili kuwa na uhakika
wa kupata matibabu wakati wowote wanapohitaji lakini pia kuhakikisha
wanatumia fursa za upimaji wa afya zinapokuwa katika maeneo yao.
Naye Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Bw. Nape Nnauye akizungumzia zoezi la upimaji
lililofanywa na NHIF uwanjani hapo, alisema kuwa ni jambo zuri kwa kuwa
mbali na watu kujua hali ya afya zao lakini watapata elimu ya namna ya
kujiunga na huduma za Mfuko.
Alitoa wito kwa vijana
kuhakikisha wanajenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kujua
hali zao kwa kuwa ndio nguvu kazi inayotegemewa katika uzalishaji wa
Taifa hili.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa NHIF, Bw. Bernard Konga alisema kuwa, Mfuko umeendesha zoezi
hilo uwanjani hapo kwa lengo la kuunga mkono juhudi zinazofanywa na
Serikali hususan katika kushughulikia tatizo la janga la tetemeko
lililotokea mkoani Kagera.
0 maoni:
Chapisha Maoni