Taasisi
ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID), imekutana na Wahariri
wa Vyombo vya Habari nchini pamoja na wadau katika kuboresha
miundombinu, semina iliyofanyika mapema jana Oktoba 19 katika ukumbi wa
mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Semina
hiyo iliyofunguliwa na mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi
na Maendeleo, Bw. Juston Lyamuya aliipongeza UTT-PID kwa namna
ilivyoweza kubobresha miundombinu pamoja na shughuli za kimaendeleo
hususani katika upatikanaji wa viwanja na hati kwa wananchi kwenye
miradi yake mbalimbali hapa nchini.
“Sote
kwa pamoja tunaipongeza UTT-PID, kwa namna inavyoendesha shughuli zake
hasa katika sehemu mbalimbali za Halmashauri, Miji na Manispaa kwani
zimeboresha miundombinu na hta wananchi kufaidika na miradi hii ambayo
ipo kwa uwazi sambamba na kuendeshwa kisasa” amesema Mgeni rasmi huyo.
Katika
semina hiyo, mada mbalimbali zimewasilishwa na wadau ikiwemo miradi ya
upamaji ardhi, miundombinu, ujenzi na fursa zilizopo katika maeneo ya
Majiji, Miji na Halmashauri hapa nchini.
Aidha,
Manispaa ya Lindi ilipongezwa kwa namna ya kipekee kufikia malengo
katika miradi yake na UTT-PID Kwani ubia wao huo umekuwa wa mafanikio
makubwa.
Naye
Mkurugezi wa Manispaa ya Lindi Jomary Satura wakati wa kuwasilisha mada
katika semina hiyo juu ya fursa za uwekezaji zinazopatikana katika
manispaa hiyo, amewaomba wananchi na wadau kujitokeza kwa wingi Manispaa
ya Lindi ilikunufaika zaidi na fursa zilizopo.
0 maoni:
Chapisha Maoni