Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya
Uratibu wa Maafa Mkoa wa Kagera wakiendelea na kikao cha kujadili na
kufanya tathimini ya hali ya athari ya Maafa ya Tetemeko la Ardhi Mkoani
Kagera.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
(Mb) akifungua kikao cha Kamati ya Uratibu wa Maafa Mkoa wa Kagera
Septemba 18, 2016, kulia kwake ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera
na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe.
Maj.Gen.Salum Kijuu akiwasilisha taarifa ya tathimini ya hali ya
waathiri wa Maafa ya Tetemeko la Ardhi mkoani hapo wakati wa kikao cha
Kamati ya Mkoa ya Uratibu wa Maafa.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya
Uratibu wa Maafa Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama wakati wa mkutano wao uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba
Mhe.Deodatus Kinawiro akichangia hoja wakati wa Kikao cha Kamati ya
Uratibu wa Maafa Mkoa wa Kagera kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano
wa Ofisi ya Mkuu Mkoa Kagera.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
0 maoni:
Chapisha Maoni