Ijumaa, 30 Septemba 2016

NAIBU WAZIRI MPINA AMUUNGA MKONO MAKONDA KATIKA ZOEZI LA KUPANDA MITI.

Posted by Esta Malibiche on Sept30.2016 in NEWS

luh1
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akipanda mti katika shule ya Sekondari ya Mama Salima Kikwete iliyopo Kijitonyama Jijini Dar es salaam ikiwa ni ishara ya kuunga mkono kampeni ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ya kupanda miti                       
luh2
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiongea na wanafunzi mara baada ya kumaliza zoezi la kupanda miti katika shule ya sekondari ya Mama Salima Kikwete.                          
luh3
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina akifafanua jambo mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mama Salima Kikwete.
……………………………………………………………..
EVELYN MKOKOI
 Kuelekea siku ya uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti jijini  Dar es salaam maarufu kama “mti wangu’, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Ameunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda katika Jitahada zake za kutunza mazingira kwa kupanda miti.
Naibu Mpina ameshiriki kwa kutangulia kupanda mti leo katika shule ya sekondani ya Salma Kikwete iliyopo kijitonyama jijini Dar es Saalam, ambapo wakala wa misitu nchini wametoa miti 600 ili kukamilisha zoezi hilo katika shule hiyo ya sekondari.
Naibu Waziri amewataka wakuu wote  wa mikoa na wilaya kuiga jitihada za Mhe. Makonda na  kuacha tabia za mazoea zilizojitokeza huko nyuma za kutoa taarifa za uwongo katika Ofisi ya Makamu wa Rais Kuwa Miti kadhaa imepandwa lakini ki uhailisia hakuna kilichofanyika.
Aidha ametoa wito kwa watendaji wa serikali wanaochakachua maaagizo ya viongozi na kusema kuwa serikali hii ipo makini hivyo kutakuwa na ufuatiliaji kwa  kila Mkoa, Wilaya na Halmashauri kwani zoezi hili la upandaji miti ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama tawala.
“Hatutavumilia kuona miti inakatwa ovyo, misitu inachomwa moto na viongozi wa serikali wakilifumbia macho suala hilo.” Alisisitiza.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugezi wa Wakala wa Misitu Nchini  Profesa Santos Silayo alisema, Taasisi hiyo imetoa jumla ya miche ya miti 8000 ili kukamilisha zoezi hilo katika jiji la Dar es Salaam, na kumpongeza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuonyesha mwanzo mpya na jitihada katika jiji la Dar es Salaam kwa kupanda miti na kutunza mazingira.
Bi Jacquline Wolper Muhamasishaji wa swala la utunzaji wa mazingira na muigizaji maarufu nchini, akishiriki zoezi hilo, kwa kupanda miti amepongeza jitihada za mkuu wa Mkoa Makonda kwa kuzunguka katika mashule mbalimbali jijini kuhamasisha zoezi hilo kwa kutoa miche ya miti

0 maoni:

Chapisha Maoni