Jumatano, 14 Septemba 2016

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

Posted by Esta Malibiche on Sept14,2016 in SIASA

bum2
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde akijibu swali wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma.
bum3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Mwigulu Nchemba akiwaeleza jambo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma.
bum4
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia mijadala bungeni leo
bum5
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akijibu swali wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma ambapo alisema kuwa serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni mbili (2) katika mfuko wa mazingira kwa ajili ya zoezi ya upandaji miti ili kutunza mazingira.
bum6
Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage  akijibu swali wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma ambapo alisema kuwa agizo la Rais Dkt. Magufuli la kuhakikisha viwanda vinavyobinafsishwa vinafanya kazi linaendelea kutekelezwa tangu Novemba 2015
bum7
Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Azzan Musa Zungu akiendesha kikao cha bunge leo mjini Dodoma
bum8
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Charles Tizeba akiwasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo wa mwaka 2016


bum1

Baadhi ya wabunge wakiingia katika ukumbi wa Bunge kuhudhuria vikao vya bunge vinavyoendeleo Mjini Dodoma.

0 maoni:

Chapisha Maoni