Posted by Esta Malibiche on Sept26.2016 in NEWS
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipokea magodoro 10 kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Mendeleo ya Wananchi
cha Kibiti, Bi. Cecilia Mfuko ukukiwa ni mchango uliotolewa na Chuo
hicho kwa Hospitali ya Kibiti. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye
mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa michezo
mjini Kibiti Septemba 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
\
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa
akimshukuru Mzee Abadallah Ngwele baada ya kupokea madawati 10
yaliyotolewa na wazee wa Kibiti katika mkutano wa hadhara aliouhutubia
kwenye uwanja wa michezo wa Kibiti, Septemba 26, 2016. Kushoto ni mkewe
Mary na watatu kulia ni Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest
Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
mkewe Mary wakiingia kwenye uwanja wa michezo wa Kibiti wilayani Kibiti
ambapo Waziri Mkuu alihutubia mkutano wa hadhara , Septemba 26, 2016.
. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………
WAZIRI MKUUkuu ,Kassim Majaliwa
ametoa wiki moja kwa Afisa Elimu Mkoa wa Pwani, Yussuph Kipengele
kupeleka walimu wa kufundisha masomo ya kidato cha tano na sita katika
shule za sekondari za Mkongo na Utete wilayani Rufiji.
Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu,
Septemba 26, 2016) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Jumba la Maendeleo wilayani
Rufiji.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo
baada ya Mbunge wa Rufiji, Muhammed Mchengelwa kumwambia kuwa wilaya
hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu wa kidato cha tano
na sita licha ya kuwa na shule.
“Hatuwezi kuwa na shule ambazo
hazina walimu, nasikia hapa anayefundisha ni Mkuu wa shule na mwalimu
mmoja tu, wakati kule Kibaha kuna walimu walmerundikana ,sasa fanya
realocation tarehe 4,Oktoba uniletee taarifa walimu wamefika
Rufiji.”,alisema Waziri Mkuu.
Akizungumzia suala la upungufu wa
watumishi wa umma kwenye sekta mbalimbali, Waziri Mkuu alisema baada ya
kazi ya uhakiki watumishi hewa itakapokamilika, serikali itaangalia
kwenye maeneo yenye upungufu na hivyo kutangaza ajira.
“Hivi sasa serikali inakamilisha
masuala ya uhakiki wa watumishi, tukimakamilisha na kujua idadi ya
watumishi na maeneo yenye upungufu tutaanza tena kuajiri, tulisitisha
kupisha kwanza kazi hii,alisema Waziri Majaliwa.
Kuhusu migogoro ya wakulima na
wafugaji Waziri, Mkuu alisema watendaji wa halmashauri na vijiji
wanapaswa kutenga maeneo ya wafugaji na wakulima na kutaka mifugo
isiongezwe kwenye maeneo ambayo hayajaruhusiwa.
Alisema wenyeviti wa vijiji
wanapaswa kusimamia utekelezaji wake katika mpango wa matumizi bora ya
ardhi na kwamba atakayeruhusu idadi kubwa ya mifugo kuingia kijijini
zaidi ya ile iliyokubalika atawajibishwa ikiwemo kufukuzwa kazi na hatua
nyingine za kisheria.
“Hatuwezi kuendelea kuwa na
watumishi wasio na nidhamu, wale wote watakaoingia mifugo zaidi ya uwezo
wa kijiji wafukuzwe kazi na kuchukuliwa hatua, lakini pia wafugaji ni
marufuko kuingiza mifugo kwenye mazao ya wakulima”alisema Waziri Mkuu.
Kuhusu ujenzi wa barabara ya lami
kwenda makao makuu ya wilaya ya Rufiji, Utete, Waziri Mkuu aliahidi
kuchukua ombi hilo na kusema bajeti ijayo litatengewa fedha kuwa ajili
ya kufanya maandalizi ya upembuzi kuona gharama yake kabla ya kutangaza
zabuni ya ujenzi.
Kuhusu utengenezaji wa madawati,
Waziri Mkuu alisema ifikapo Oktoba 30, mwaka huu kila wilaya nchini
inapaswa iwe imekamilisha utengenezaji wa madawati hayo kwenye shule
nchini.
Aidha, alisema ipo miradi mingi
inayoendeshwa kwa maslahi binafsi ukiwemo mradi wa Bonde la
Rufiji(RUBADA), ambao wamebaini kuna ubabaishaji mkubwa, hivyo
wamepeleka timu ya wataalamu kuhakiki ili wale wabadhirifu wachukuliwe
hatua.
0 maoni:
Chapisha Maoni