Jumanne, 27 Septemba 2016

Wodi ya wazazi Muhimbili kuwekewa luninga


Wanachama wa Umoja wa Vijana Kibosho (UVIKI) wametoa luninga moja,deki,na king’amuzi cha azam katika Hosptali Ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya wodi ya wazazi pamoja na kuchangia damu.
Akizungumza wakati wa kutoa televisheni hiyo pamoja kuchangia damu Mwenyekiti wa umoja huo Marceli mushi , amesema kuwa atawaamasisha vikundi vingine kuchangia katika huduma za afya ili kusaidia watanzania wengine wenye mahitaji.
“Tumekuja hapa tumejifunza mengi na tumepata elimu huko kwenye jamii tunakoenda kukutana na watu tutafikisha ujumbe ili nao waweze kujitolea kuchangia kuokoa maisha ya watu,” alisema Mushi
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha ameshukuru umoja huo kwa kujitolea kuchangia damu na kutoa luninga hiyo itakayo tumika kutoa elimu kwa kinamama
“Tunashukuru kwa kweli kwasababu mahitaji ya damu ni makubwa hasa kwa kina mama wajawazito na watoto na tunatumia chupa 90 mapka 110 kwa siku,” alisema Aligaesha.
Naye Kaimu Meneja wa wodi hiyo Bi. Stella Medadi amesema luninga hiyo itatumika kwa kuweka vipindi vitakavyosaidia kutoa elimu ya uzazi,lishe na maandalizi ya mama mjamzito pamoja na vidokezo vya hatari kwa mama wajawazito.
Na Sheila Simba -Maelezo

0 maoni:

Chapisha Maoni