Posted by Esta Malibiche Oct 1.2016 in SIASA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
mkewe Mary wakiwapungia akiwapungia wananchi wa Dodoma baada ya kuwasili
kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea ufunguo ikiwa ni ishara
ya kukaribishwa Dodoma na Meya wa Manispaa ya Dodoma Jafar Mwanyemba
katika mapokezi yaliyofanyika kwenye makazi yake , Mlimwa Septemba 30,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha ufunguo aliokabidhiwa
na Meya wa Manispaa ya Dodoma, Jafar Mwanyemba (kushoto) kuashiria
kupokewa rasmi kwenye manispaa hiyo. Makbidhiano hayo yalifanyika kwenye
makazi yake eneo la Mlimwa Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na
wazee wa Dodoma baada ya kukaribishwa kimira na wazee hao Septemba 30,
2016.
Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizawadiwa kimira na
wanawake wa Dodoma ikiwa ni ishara ya kumkaribisha karika Manispaa hiyo,
Septemba 30, 2016.
Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizawadiwa kimira na
wanawake wa Dodoma ikiwa ni ishara ya kumkaribisha karika Manispaa hiyo,
Septemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa na mkewe Mary wakiagana na
watuimishi wa Makazi ya Waziri Mkuu ya Dar es salaam kabla ya kuondoka
kuelekea Dodoma Septemba 30, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
mkewe Mary wakisalimiana na Madiwani wa Manispaa ya Dodoma baada ya
kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
mkewe Mary wakisalimiana na Madiwani wa Manispaa ya Dodoma baada ya
kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kasim Majliwa akiwapungia wananchi baada ya
kuwasili kwenye makazi yake mjini Dodoma Septemba 30, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wa Dodoma wakimshangilia
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye makazi
yake eneo la Mlimwa Septemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………………
Waziri MKUU
Kassim Majaliwa amesema kuanzia sasa mtu yeyote mwenye shida ya kuonana
naye itabidi amfuate Dodoma na kwamba atarudi Dar es Salaam pindi
akiitwa na Mheshimiwa Rais au Makamu wa Rais.
Ametoa kauli hiyo leo jioni (Ijumaa, Septemba 30, 2016) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali na wakazi wa mji wa Dodoma waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili mjini hapa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa Julai 25 kuwa atahamia Dodoma ifikapo Septemba mwaka huu.

“Tukio hili la
kuhamia Dodoma si la mzaha, hakuna siasa na wala si jaribio.
Tumeshakeleza. Kama kuna waliokuwa wanafiria kwamba halitekelezeki
watambua kwamba tayari tumeshafika. Na kuanzia sasa atakayetaka huduma
ya Waziri Mkuu
Waziri
Mkuu amesema Dodoma si ndogo kama baadhi ya watu wanavyodai na kwamba
huduma zilizopo zinatosha kukidhi mahitaji ya sasa. “Mkakati uliopo wa
kupanua huduma za tiba, maji, umeme na masoko utawezesha watumishi wote
kuishi bila bugudha yoyote.”
“Awamu ya kwanza inaanzia Septemba hadi Februari mwakani. Mimi nimeshatangulia na wanaofuata ni mawaziri na manaibu wao wote, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wote. Natambua kwamba wote wana nyumba za kuishi na kama wapo ambao hawana hawazidi asilimia tano na nyumba zipo

Amewataka
watumishi wote wa Serikali watambue kwamba safari imeshaanza na kila
mmoja ajipange, na akarudia wito wa Mheshimiwa Rais kwamba atakayegoma
kuhamia Dodoma atakuwa amejifukuza kazi.
Waziri Mkuu
amewataka watendaji wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA)
wasifanye kazi kwa mazoea, bali wabadilike na kwa kuwa amehamia Dodoma
ameahidi kuafuatilia kwa karibu zaidi.
Mapema
akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Nchi (OWM SUBKAV), Jenista
Mhagama amesema kilichofanyika leo ni uthibitisho kuwa yale ambayo
Serikali ya Awamu ya Tano iliahidi sasa hivi imeanza kuyatekeleza.
“Tuliahidi kukusanya kodi, tuliahidi elimu bure, tuliahidi kupambana na mafisadi, tuliahidi kuondoa watumishi hewa, tuliahidi kuifufua ATCL na kununua ndege mpya na yote tumetekeleza,” amesema.
“Tuliahidi kukusanya kodi, tuliahidi elimu bure, tuliahidi kupambana na mafisadi, tuliahidi kuondoa watumishi hewa, tuliahidi kuifufua ATCL na kununua ndege mpya na yote tumetekeleza,” amesema.
Naye
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. George Simbachawene amesema
uamuzi wa kuhamia Dodoma ni uthibitisho kuwa viongozi wetu kweli
wamedhamiria kutekeleza ahadi ya Baba wa Taifa ya kuhamishia makao makuu
ya nchi hapa Dodoma.
“Dodoma imeanza kuchangamka na hii ni fursa tosha kwa mkoa wetu kubadilika. Tushirikiane na CDA kuijenga Dodoma mpya. Kitendo cha Mheshimiwa Waziri Mkuu kuingia Dodoma leo hii maana yake ni kwamba Serikali iko rasmi Dodoma,” amesema.

Hafla hiyo
ilihudhuriwa na Manaibu Waziri Anthony Mavunde na Dk. Ashatu Kijaji,
Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais (Utumishi),
Wakuu wa Wilaya za Mkoa huo, wazee wa mkoa huo, viongozi wa dini,
viongozi wa taasisi zilizoko mkoani na baadhi ya wananchi.
0 maoni:
Chapisha Maoni