Meneja wa kiwanda cha TBL Mbeya,Jemedari Waziri akiongea na ujumbe wa waandishi wa habari waliotembelea kiwanda
Mtaalamu wa
Mafunzo wa Kiwanda cha Bia cha TBL- Mbeya, Christian Kivyiro akitoa
maelekezo kwa waandishi wa habari wanawake wa Mkoa wa Mbeya,
walipotembelea kiwanda hicho jana ili kujifunza namna kinavyofanya kazi
Mtaalamu wa
Mafunzo wa Kiwanda cha Bia cha TBL- Mbeya, Christian Kivyiro
akiwaonyesha Shahiri waandishi wa habari wanawake wa Mkoa wa Mbeya,
walipotembelea kiwanda hicho ili kujifunza namna kinavyofanya kazi
Fundi Sanifu wa
maabara ya kiwanda cha Bia cha TBL-Mbeya, Phili Said (kulia) akitoa
maelekezo namna pombe inavyopimwa katika maabara yao kwa waandishi wa
habari wanawake wa Mkoa wa Mbeya.
Waandishi wakiwa pichani wakiwa wameshikilia ngao na cheti cha tuzo za ushindi wa kiwanda bora barani Afrika
…………………………………………………….
-Wafurahia mafanikio yake
Siku chache baada ya kiwanda cha
bia cha TBL Mbeya kutangazwa kuwa kiwanda bora barani Afrika,pongezi kwa
mafanikio hayo zimekuwa zikitolewa kutoka makundi mbalimbali ya kijamii
mkoani humo na kupokea maombi ya kutembelewa kwa ajili ya mafunzo na
kujionea jinsi kinavyoendesha shughuli zake.
Moja ya kundi lililoguswa na
mafanikio hayo na kutembelea kiwanda hicho ni wanachama kutoka Chama Cha
Waandishi wa Habari Wanawake mkoani humo ambao baadhi ya wanachama wake
wametembelea kiwanda na kupata fursa ya kutembezwa idara mbalimbali
kiwandani hapo na kuongea na Meneja wa kiwanda,Mhandisi Jemedari Waziri.
Waziri aliwaelezea waandishi hao
kuwa siri ya mafanikio hayo ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni
kuanzia kwenye mitambo ya uzalishaji mpaka kwenye wafanyakazi
walioajiriwa na kiwanda bila kusahau mifumo ya uendeshaji viwanda ya
kisasa iliyowekwa na kampuni.
Alisema kiwanda kitaendelea
kushirikiana na serikali na wadau wengine mkoani humo katika miradi
mbalimbali ya kubadilisha jamii hususani katika sekta ya utunzaji
Mazingira na kulinda vyanzo vya maji.
0 maoni:
Chapisha Maoni