Jumanne, 13 Septemba 2016

Wafanyakazi TBL Group walivyoshiriki tamasha la mashindano ya mbuzi

mbu1
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin (aliyeshika mbuzi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi baada ya mbuzi wao kushinda
mbu2
Meneja wa bia ya Kilimanjaro,Pamela Kikuli akikabidhi hundi ya udhamini
mbu3
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kwenye tamasha
mbu4
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakiburudika na kinywaji cha Kilimanjaro Lager.
mbu5
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa waandamizi wa kampuni hiyo kwenye tamasha
mbu6
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin akiongoza wafanyakazi kusheherekea ushindi .
mbu7
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin akiongoza wafanyakazi kusheherekea ushindi .
mbu8
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja katika mbio hizo za mbuzi.
…………………………………………………
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya TBL Group,Roberto Jarrin aliungana na wafanyakazi wa kampuni hiyo katika tukio muhimu la kuchangisha fedha za kukabiliana na changamoto za kijamii kupitia mchezo wa mashindano ya mbuzi uliofanyika kwenye viwanja vya Farasi vilivyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mwaka huu kampuni imedhamini mashindano haya yaliyolenga kukusanya fedha za kusaidia vituo vya kulelea watoto wenye mahitaji maalum kupitia bia yake ya Kilimanjaro.
Kama ilivyo moja ya sera ya kampuni inayoelekeza wafanyakazi wake kutenga muda wao kushiriki katika masuala ya kusaidia jamii,wafanyakazi wa TBL Group walijitokeza kwa wingi na walikuwa na furaha  wakati wote ya kushiriki tukio hili muhimu linalolenga kuleta mabadiliko kwenye jamii.

0 maoni:

Chapisha Maoni