Mbunifu wa mavazi kutoka marekani Marc Jacobs aonesha historia ya mitindo ya nywele kupitia wana mitindo wake ambao aliwavalisha kulingana na miaka yote aliofanya ubunifu wake kuanzia mwaka 1996 mpka leo, huku akichukua kofia ya mbunifu bora wa mwaka katika mitindo ya nywele.
Marc Jacobs amesema kwamba amekua akivutiwa na nywele za wanawake hivyo kumpelekea kujihusisha na kutengeneza mitindo mbalimbali ya nywele na kumuwezesha kufanikiwa au kufikia hapa alipo sasa.
“kati ya vitu vinavyompendezesha mwanamke ni nywele hivyo zimekuazikinivutia na kuibuka na mbinumbalimbali kila siku katika kuboresha na kufanya kitu cha tofauti kuvutia watu wengi zaidi.” Amesema Marc   
Aidha taarifa zimesema kwamba Jacob amekua akiongoza katika ubunifu bora kwa muda mrefu sasa kupitia kampuni yake ya mavazi iitwayo “marc Jacobs” yenye maduka ya nguo 200 katika zaidi ya nchi 80 duniani, huku akifanya kazi na lebo ya kampuni kubwa ya nguo “lousi Vuitton”.
1fed76445716e9acc0b06923716a3cb8 00c5b42c3fd25557798884768d268afd 4d78654ac43707ec3569d9ad461801cc 5b08931da47078031ceb09de93e1d571