Ijumaa, 30 Septemba 2016

MKUU WA WILAYA YA BARIADI FESTO KISWAGA AZINDUA MSIMU WA KILIMO NA KUGAWA MBENGU KWA WANANCHI .

Posted by Esta Malibiche on Sept30.2016 in NEWS

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga (Kulia) akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa msimu wa kilimo wilayani humo 2016/17, (kulia) ni Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya hiyo Duka Mashauri Mapya.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga akigawa Mbegu bure kwa wananchi wa kata ya Nkololo, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Msimu wa kilimo wilayani humo 2016/17.

Mkuu wa wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu akiongea na wananchi wa kata ya Nkololo wilayani humo, wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo wilayani humo 2016/17.

Wananchi wa kata ya Nkololo wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga.( hayupo pichani).




Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga akigawa Mbegu kwa Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Bariadi Robert Rweyo (katikati) pamoja na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya Duka Mashauri Mapya.




Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga akigawa Mbegu kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo, wakati wa zoezi la uzinduzi wa msimu wa kilimo wilayani humo 2016/17.

Add caption

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga akigawa Mbegu bure kwa wananchi wa kata ya Nkololo, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Msimu wa kilimo wilayani humo 2016/17.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga akigawa Mbegu bure kwa wananchi wa kata ya Nkololo, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Msimu wa kilimo wilayani humo 2016/17.

 

Mkuu wa wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga amewataka wananchi  kutumia mvua zinazoanza kunyesha  kupanda mbengu bora za mazao ya chakula na biashara ili kujipatia chakula pamoja na kukuza uchumi wao na jamii kwa ujumla.


Kauli hiyo ameitoa jana wakati akizungumza na wananchi katika  uzinduzi wa msimu mpya wa kilimo 2016/17 uliofanyika katika kijiji cha Nkololo wilayani Bariadi na kugawa mbegu bure  kwa wananchi.
 Kiswaga alisema kuwa ofisi yake imejipanga kuhakikisha wananchi wanalima na kupata mazao kwa kiwango kikubwa ili kuweza kuondokana na janga la njaa ikiwa pamoja na kuachana na utamaduni wa kuomba chakula serikalini.

Kiswaga alisema kuwa kila kaya inatakiwa kuhakikisha inalima hekari nne za mazao ya chakula kama mahindi,maharagwe pamoja na mazao ya biashara kama Mbaazi, Choroko pamoja na Pamba.
   huku kila hekari moja ikipandwa  zao moja, ili kuondokana na changamoto ya ughaba wa chakula.


Alisema kila kata inatakiwa kulima mazao hayo katika msimu huu na misimu mingine mbeleni, kama hatua ya kuazia katika mpango ambao alisema ameuanzisha  wa ushirikishwaji wa wananchi katika kilimo chini ya kauli mbiu isemayo '''KILIMO HUONDOA UMASIKINI NA NJAA'''

Aidha alisema kulima mazao hayo manne itakuwa la
" Sitamvumilia mtu yeyote atakaebainika anasambaza mbolea feki kwa wakulima pamoja na kuuza mbegu zisizo na ubora,nitamchulia hatua za kinidhamu
'''''alisema Kiswagazima, ambapo aliwataka wananchi kutoa taarifa ofisini kwake au kwa viongozi wengine mara watakapobaini wafanyabiashara au makampuni yatakayodiriki  kusambaza pembejeo feki za kilimo''''''alisema Kiswaga

 '''''''''''Ninawaomba wananchi wote tuungane pamoja kuunga mkono mpango  huu ambao tunaanza na mazao ya aina nne, niwatake toeni taarifa kwa watu watakaowapatia mbegu na madawa feki, watalam wa halmashauri lazima kusimamia mpango kwa wananchi ili kuweza kuzalisha kwa kiwango kikubwa msimu huu" Alisema Kiswaga.
Awali Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Bariadi Duka Mashauri Mapya, alisema kuwa wananchi wa wilaya hiyo hasa wanaopakana na hifadhi ya Taifa Serengeti wamekuwa wakipata kero kubwa kutoka kwa wanyama hasa tembo kwa kuaribu mazao yao.
Alimuomba Mkuu wa wilaya katika kutekeleza mpango huo suala la wanyama hao lazima kuangaliwa kwa kiwango kikubwa ikiwa pamoja na kupambana na watu wanaosambaza mbegu na madawa feki.

0 maoni:

Chapisha Maoni