Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla ameagiza waajili wote nchini kutoajili wataalamu
wasio sajiliwa na wataalamu wa Baraza la Maabara za Afya nchini ili
kuepuka kuajili wataalam hewa.
Dk.
Kigwangalla ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Baraza la
Wataalamu wa Huduma za Maabara za Afya tukio lililofanyika Jijini Dar es
Salaam ambapo Naibu Waziri alikuwa mgeni rasmi huku akitoa vyeti kwa
wajumbe wa Baraza hilo waliomaliza muda wao pamoja na wajumbe wapya.
Akipongeza
Baraza hulo la Maabara, amesema kuwa licha ya kuwa ni la siku nyingi,
ambapo amelitaka kuhakikisha wanashirikiana na Mamlaka zingine husika
kusimamia ubora wa wataalamu kusimamia vyuo husika katika kuwapata
wataalam hao.
Pia
amewataka wataalamu wa Maabara waliosajiliwa kwa sheria ya 12 ya 1997,
wajisajili tena upya kwa sheria mpya ya namba 22 ya mwaka 2007 kama
ilivyoelekezwa ili wapate vyeti vipya.
Mwisho
amewaagiza wataalamu woye wa maabara waliosajiliwa wanalipia ada ya
usajili kila mwaka ili kuendelea kupata kibali cha kuendelea kutoa
huduma cha maabara kwa mwaka mzima ili baraza hilo liweze kujiendesha.
“Ili
muwe wataalam, lazima muwe na chombo kama hichi. Hivyo katika msingi
huo nyie wataalum wenyewe mutakiwa kujiongeza katika kuhakikisha
munapata fedha kwa kuchangia/kuchangishana muweze kujindesha kama
yalivyo mabaraza mengine” amesema Dk.Kigwangalla.
Baraza
la Wataalamu wa Maabara za Afya, ni chombo cha kisheria kilichowekwa na
Serikali ili kuwatambua na kuwasajili Wataalamu wa Maabara za Afya ya
Binadamu, kusimamia ubora wa utoaji wa huduma za uchunguzi wa magonjwa
ya binadamu, kuchukua hatua za kisheria kwa wakiukaji wa sheria, na
kushauri Serikali katika kuboresha huduma za maabara kwa wagonjwa.
Taaluma
ya Maabara za Afya ni kati ya taaluma nyeti katika tasnia ya tiba na
Sekta ya Afya kwa ujumla. Kwa kuwa ndio inayotoa dira ya tiba sahihi
kwa wagonjwa wanaohitaji tiba. Isitoshe, magonjwa ya milipuko na
magonjwa yanayoibukia, mfano homa ya bonde la ufa, Dengue na Ebola
yanahitaji taaluma ya maabara kuweza kuyabaini na kuyadhibiti.
Aidha,
tafiti nyingi za magonjwa ya binadamu duniani zinahitaji taaluma ya
Maabara kuweza kupata ushahidi wa kisayansi ili kupata tiba sahihi kwa
wagonjwa na kudhibiti au kupata kinga kwenye jamii. Hivyo, Baraza hili
lina jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa, taaluma hii inakuwa na ubora
unaostahili kwa faida ya Taifa zima kwa ujumla.
Katika
kutekeleza agizo hilo, Wizara itandelea kuongeza nguvu katika juhudi za
kufuatilia vyuo vyote vilivyohusika na vyeti vya kugushi. Ambapo
ameomba Kamisheni ya Vyuo Vikuu (TCU) na Taasisi ya Taifa ya Elimu ya
Ufundi (NACTE) kuwa makini katika usaili na ufuatiliaji wa ubora wa
taaluma zinazotolewa katika vyuo wanavyovisimamia na kuvisajili.
“Tushirikiane
kuhakikisha kuwa hakuna Taasisi au Mtu Binafsi, atakayefungua au
atakayetoa mafunzo ya taaluma bila kusajiliwa kisheria. Aidha,
nawakumbusha waajiri wote wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, wazingatie
kutowaajiri watalaamu ambao hawajasajiliwa” alimalizia Dk. Kigwangalla.
Mganga
Mkuu wa Serikali Dkt. Mohamed Bakari Kambi akifungua mkutano huo wa
uzinduzi wa Baraza la Wataalamu wa Huduma za Maabara za Afya nchini.
Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wataalam wa Maabara za Afya nchini waliomaliza muda wao wakifuatilia tukio hilo
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia tukio hilo
Baadhi ya wajumbe wapya wa Baraza hilo wakijitambulisha
Meza
kuu: Dkt. Magreth Mhando, Mkurugenzi wa Idara ya Tiba, Naibu Waziri wa
Afya Dk.Kigwangalla na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Mohamed Bakari Kambi
katika tukio hilo
Picha ya pamoja ya Wajumbe wa Baraza la Wataalam wa Maabara za Afya wakiwa na mgeni rasmi Naibu Waaziri wa Afya Dk.Kigwangalla.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa Habari juu ya hali ya
wataalamu wa Maabara nchini. (Picha zote na Andrew Chale
0 maoni:
Chapisha Maoni