Kamanda wa Jeshi la zima moto mkoani Irionga Kennedy Komba akizungumza na blog ya KALI YA HABARI katika mahojiano maalum kuhusu mikakati iliyowekwa na jeshi hilo kupamnaba na majanga ya moto katika shule za Msingi,Sekondari na Vyuo,Mkoani Iringa.
Na Esta Malibiche
Iringa
Kamanda wa jeshi la zima moto mkoa wa Iringa
Kennedy Komba amewataka wamiliki wa shule Mkoani Iringa kuhakikisha
wanafunga vifaa vya zima moto ili kujiadhari na majanga ya moto mara yanapotokea.
Kauli hiyo ameitoa ofisini kwake wakati akifanya
mahojiano maalum na Blog hii ya KALI YA HABARI juu ya utoaji Elimu
katika shule mbalimbali ili ziweze kujinginga na majanga ya moto mara
yanapotokea.
Komba alisema katika kuuweka mkoa wa Iringa salama na janga
la moto,jeshi la zimamoto linaendelea kutoa mafunzo katika shule za msingi na
sekondari na vyuo ili kuondoa tatizo la
janga la moto kwa wanafunzi wawapo mashuleni.
Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwapa uelewa jinsi
kuepukana na majanga ya moto shuleni.Na endapo janga likitokea wanaweza
kukabiliana nalo na kujiokoa pasipo kuleta madhara yeyote.
‘’’’’’’ Shule nyingi zinaumeme ambao ni chanzo
kikubwa cha moto lazima tuwe na
tahadhari.Pia katika shule tulizotoa elimu kuhusu kujiadhari na majanga ya
moto,jumla ya vijana 1840 wamepata mafunzo na mwitikio ni mkubwa.Tumeanza na
Manispaa ya Iringa,tutahakikisha tunazifikia
shule zote zilizopo katika kila wilaya za mkoa huu’’’’’’’alisema komba
Kamanda alisema vifaa vinavyotakiwa kuweka katika
shule za Msingi,Sekondari na Vyuo kwa ajili ya kujikinga na majanga ya moto ni
pamoja na Ndoo ya mchanga mkavu,Fire Extingusher,Pamoja na viashiria vinavyotoa
sauti kama king’ola.
Aidha kamanda Kamanda Komba amesihi wamiliki wa vyombo
vya usafiri na usafirishaji kuhakikisha wanapeleka vyombo vyao kufanyiwa ukaguzi na
kupewa fomu maalum ya ukaguzi,na kununua vifaa vya kudhibiti janga hilo ili
kuondokana na athari.
‘’’’Kinga ni bora
kuliko tiba.Tujiwekee utaratibu wa kuweka kinga kabla ya janga halijatoke’’’’alisema
Kamanda Komba
MWISHO
|
0 maoni:
Chapisha Maoni