-Kimedhihihirisha kuwa Tanzania yenye viwanda inawezekana
Wakati
serikali ya awamu ya tano inajipanga kuifanya Tanzania nchi ya viwanda
tayari dalili njema zimeishajitokeza kuwa watanzania tukiamua tunaweza
kwa kuwa kiwanda kinachoshikilia rekodi ya ubora barani Afrika ni
kiwanda cha kutengeneza Bia cha TBL kilichopo katika kitongoji cha
Iyunga mkoani Mbeya.
Kwa
mara nyingine tena baada ya kushindanishwa na viwanda vikubwa
vipatavyo 21 barani Afrika,mwishoni mwa wiki iliyopita TBL Mbeya
imeibuka kinara na kutangazwa kuwa kiwanda bora barani Afrika kati ya
viwanda vilivyopo chini ya kampuni kubwa yenye viwanda vya kutengeneza
bia duniani ya SABMiller na kimelinda rekodi yake kilichokuwa
kinaishikilia.
Rekodi
hii inaenda sambamba na dhamira ya serikali ya kuifanya Tanzania nchi
ya viwanda na inadhihirisha kuwa uwekezaji wa viwanda sio lazima ufanywe
maeneo ya mijini kama ambavyo ilikuwa imezoeleka kwa muda mrefu.
Wafanyakazi
wa Kiwanda cha Bia cha TBL- Mbeya, wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa
na kombe na cheti cha ushindi baada ya kiwanda hicho kutwaa tuzo ya
kuwa kiwanda bora na kushika nafasi ya kwanza Afrika kati ya viwanda 21
vya bia barani Afrika muda mfupi baada ya Meneja wa Kiwanda hicho,
Jemedari Waziri kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe
(SIA)-Mbeya akitokea Afrika ya Kusini.
Mhandisi
Jemedari Waziri,Meneja wa kiwanda hiki akiongelea mafanikio haya
alisema kuwa anajivunia ushindi huu kwa kuwa ni uthibitisho halisi kuwa
watanzania tunaweza kufanya vizuri na kuleta maendeleo kwa kasi
tukiamua.
“Tunaposema
ubora wa kiwanda tunaamaanisha ubora wa bidhaa tunazozalisha,teknolojia
tunazotumia,raslimali watu tuliyonayo,mchango wa kiwanda kwa serikali
na jamii iliyotuzunguka bila kusahau utunzaji wa mazingira ambayo ni
moja ya nguzo ya kampuni yetu”.Alisema.
Wafanyakazi
wa kiwanda cha Bia cha TBL- Mbeya, wakionyesha kombe na cheti cha
ushindi mitaani wakati wa mapokezi ya Meneja wa Kiwanda hicho.
Aliongeza
kuwa ushindi huu ni kwa wana Mbeya wote na wana kanda ya Nyanda za Juu
Kusini “Tunawashukuru wateja wetu wote kwa kutuunga mkono wakati wote na
tutaendelea kuwaletea bidhaa bora kwenye soko na kubuni miradi
mbalimbali ya kijamii itakayosaidia kuleta mabadiliko”.Alisema
Jemedari
pia alisema ushindi huu unatokana na jitihada za pamoja kutoka kwa
wafanyakazi wote wa kiwanda na TBL Group kwa jumla na anafurahi kuona
kiwanda kinaendeshwa na watanzania asilimia kubwa ikiwa ni vijana wenye
vipaji vya ajabu na waliobobea katika fani mbalimbali.
Wafanyakazi wa TBL Mbeya wakiwa nje ya lango kuu la kuingilia ofisini kwao.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Mbeya wakiangalia kombe la ushindi.
Baadhi ya wafanyakazi wakipata chakula katika hafla ya kusheherekea ushindi.
0 maoni:
Chapisha Maoni