Na Mahmoud Ahmad,Arusha
Jumla ya Tsh.154 milion wameapatiwa waalimu 701wa
shule za msingi na sekondari kutoka kwenye fedha ambazo zilitakiwa
kulipa posho za nauli na simu za madiwani wa jiji la Arusha.
Akiongea na wanahabari ofisini kwake jijini hapa
mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro alisema kuwa kutokana na
malimbikizo ya fedha za likizo,kufiwa,nauli, uhamisho waliokuwa wanadai
walimu ndio maana tumeamua kuwalipa ili waweze kufanyakazi ya kufundisha
watoto wetu kwa moyo.
Daqqaro alisema kuwa baada ya kikao na mkuu wa
mkoa Mrisho Gambo na waalimu wa shule 48 za jiji la Arusha, na kuagizwa
kuhakikisha walimu wanalipwa stahiki zao ndani ya wiki mbili na agizo
hilo tumelitiza na walimu wamelipwa fedha zao.
Alisema kuwa fedha zilizolipwa waalimu hao
tumezitoa kwenye fedha zilizokuwa wakijilipa madiwani posho za usafiri
na posho za simu na kuzielekeza fedha hizo kutatua kero ya waalimu na
mwisho wa siku vijana wetu wapate elimu stahiki bila manung’unuko kutoka
kwa waalimu.
”Hapa napenda tusiingize ushabiki wa kisiasa
katika hili na tuache kuzusha maneno maneno yanayaashiria uvunjifu wa
amani kama kweli fedha hizo wanadai walifuta iwaje leo waendeleze
maneno”alisema DC Daqqaro.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ipo
kuhakikisha wananchi walio wengi wanaondolewa kero zao kwa wakati na
kuondosha kabisa kero mbali mbali ndani ya jamii ikiwemo waalimu kupewa
stahiki zao kwa wakati.
Akawataka waalimu hao kuhakikisha malengo ya mkoa
kuongeza ufaulu yamefikiwa kwa kufanyakazi kwa moyo huku serikali
ikiendelea kumalizia malalamiko mbali mbali ya waalimu wa mkoa wetu.
Malipo hayo ya waalimu 701yametokana na agizo la
mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwataka dc na mkurugenzi wa jiji
la Arusha Athman kihamia kuhakikisha malalamiko ya waalimu walioyatoa
kwenye mkutano wao yanatekelezwa ndani ya wiki mbili .
0 maoni:
Chapisha Maoni