Kali ya habari
Posted by Esta Malibiche on Sept29.2016 in NEWS
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
SERIKALI
imeanza kutenga fedha sh. bil.2 ambazo tayari zimeshapelekwa wizara ya
ujenzi ,ili kujengwa gati itakayohudumia wananchi wa Nyamisati wilayani
Kibiti,Mafia na Rufiji.
Aidha
serikali inafanya utaratibu wa kutafuta boti moja kubwa ambayo itaweza
kuhimili nguvu ya maji na kukatisha katika maeno hayo.
Waziri
mkuu Kassim Majaliwa aliyazungumza hayo kwenye mkutano wa hadhara wa
wananchi huko Nyamisati wilaya ya Kibiti,mkoani Pwani.
Alisema
serikali imedhamiria kuimarisha na kuondoa kero iliyopo kwasasa
wanayopata wananchi baada ya gati la awali kubomoka kutokana na
kushindwa kuhimili nguvu ya maji.
Alisema
kipindi cha nyuma halmashauri yenyewe ilijenga gati hiyo kwa kiasi cha
sh.mil.400 lakini ilibomoka kutokana na wingi wa maji .
“Wilaya
ya mafia waliizungumzia vizuri sana kuwa ni tumaini lao,na mimi
nilidhani watazungumzia kitu kipya lakini wameipenda sana
Nyamisati,kwahiyo wakizungumza kitu ambacho nakifahamu,lakini serikali
inajua gati hii inatumika na wilaya yote ya Mafia hivyo ni lazima
tuimarishe”alisema Majaliwa.
Majaliwa
alisema kwasasa watu wanapata shida ya kukwida nguo ndipo upande boti
lakini anatarajia baada ya kujengwa gati hiyo kero hiyo itabaki
historia.
Alieleza
kuwa gati hiyo itajengwa na fedha imeshatengwa na kupelekwa wizara ya
ujenzi waende kushughulikia kuijengajenga kwani barabara ni kubwa na
gati ni tegemeo la wilaya yote ya Mafia.
Hata hivyo alisema mbinge wa
jimbo la Kibiti,Ally Ung’ando ,amekuwa akisema mara kwa mara na
kung’ang’ania juu ya suala hilo hivyo majibu yake ni hayo wananachi wawe
na subira.
Alisema
masuala ya gati yanaenda sambamba na miundombinu ya barabara ambapo
alikiri kwasasa serikali ilishindwa kutenga fedha kwa ajili ya barabara
ya Bungu-Nyamisati.
Alisema
kwasasa wataiimarisha kwa kiwango cha changalawe ili iweze kutumika
wakati wote licha ya hamu ya wilaya kutaka ijengwe kwa kiwango cha lami
barabara hiyo.
Majaliwa
alieleza kwa mwaka huu,wameendelea kulipa madeni ya barabara kuu
ikiwemo Dar es salaam,Lindi,Masasi kwani mkandarasi alikuwa akidai fedha
kutoka Masasi ,Tunduru,Namtumbo,Songea, Mbinga na Mbababei.
“Kuna
barabara inayotoka Mbeya kwenda mikoa ya Songwe ,Tunduma,Sumbawanga
,Katavi hadi Uvinza- Kigoma kuunganisha barabara ya kutoka Kigoma
–Tabora ambayo tayari ina lami ,tunafanya hivyo ili kuwezesha barabara
mzunguko nchi nzima na zoezi hilo tutalikamilisha “
“Tunafanya
hivyo kwasababu ya kuijenga barabara ya kutoka Dodoma kupitia Kondoa
kwenda Babati mjini kwahiyo watu wa Dodoma watakwenda Arusha kwa ukaribu
na wa Arusha watakwenda makao makuu ya nchi kwa ukaribu zaidi”
‘Pia
kuimarisha barabara kutoka Kigoma kwenda Kasulu,Kibondo na kutokeza
Nyakanazi ili kuunganisha barabara ya kutoka
Ngara,Bukombe,Kahama,Shinyanga hivyo huo ndio mkakati wa serikali.
Majaliwa
alielezea kuwa mpango ni kukamilisha barabara zote kuu nchini kwa
kiwango cha lami ,kisha za ndani ya mikoa ambazo hazijakamilika na
baada ya hapo za wilaya ikiwemo Bungu-Nyamisati,Nyamwage-Utete na
Kilimani –Mloka.
Aliwahidi wananchi na mbunge wa Kibiti kuwa barabara hizo ni muhimu hivyo serikali haiwezi kuwaangusha .
Majaliwa
alisema wanaendelea kuwabana wabadhilifu wa fedha na wafanyabiashara
kulipa kodi ili fedha hizo ziweze kuwatumikia wananchi kwenye huduma
mbalimbali za kijamii ikiwemo kuboresha na kuimarisha miundombinu ya
barabara.
Awali
mbunge wa viti maalum na mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake mkoani
Pwani,Zainab Vullu alieleza kero kubwa ya ukosefu wa gati hali
inayosababisha wananchi kupata kero.
0 maoni:
Chapisha Maoni