Jumapili, 18 Septemba 2016

Waziri Nape atoa million tano kwa Serengeti Boys.

ser1
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza leo Jijini Dar es Salaam na wachezaji wa Serengeti Boys katika hafla fupi ya kuwakabidhi Shilingi Milioni Tano kama motisha kabla ya mechi ya leo dhidi ya Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
ser2
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Bw. Jamali Malinzi akitoa maelezo juu ya maaandalizi ya mechi kati ya Serengeti Boys na Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
ser3
Kocha wa Serengeti Boys Bw. Bw.Bakari  Shime akimshukuru Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) kwa kuwapa motisha wachezaji kabla ya mechi kati ya Serengeti Boys na Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
ser4
Nahodha wa Serengeti Boys Bw. Issa Abdi Makame akiahidi kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) kuibuka na ushindi dhidi ya Congo-Brazaville katika mechi itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
ser5
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akimkabidhi Millioni tano Nahodha wa Serengeti Boys Bw. Issa Abdi Makame kama motisha kabla ya kabla ya mechi ya leo dhidi ya Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
ser6 ser7
Baadhi ya wachezaji wa Serengeti Boys wakimsikiliza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) katika hafla fupi kabla ya mechi yao dhidi ya Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
(Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM) 
……………………………………………………………………….
Na Shamimu Nyaki- WHUSM.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametoa kiasi cha shilingi million tano kwa timu ya Serengeti Boys kama motisha katika mchezo wao dhidi ya Congo Brazivile utakayochezwa leo katika Uwanja wa Taifa Jjijini Dar es Salaam.
Akikabidhi pesa hizo leo Jijini Dar es Salaam  Mhe. Waziri Nape amewataka wachezaji hao kujituma zaidi katika mechi hiyo ili wapate ushindi utakaowawezesha kufuzu   katika fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana  chini ya miaka 17 .
“Watanzania wote tupo  pamoja na nyie endeleeni kujituma kama mlivyofanya katika hatua ya kwanza na ya pili,  Sisi kama  Serikali tunawaunga mkono na tunawatakia heri ili mlete heshima kwa Taifa.”Alisema Mhe. Nape.
Kwa upande wa Kocha wa Timu hiyo Bw.Bakari  Shime amemuhakikishia Waziri na Watanzania kwa ujumla kuwa mechi ya leo watahakikisha wanapata ushindi kwani wamejiandaa vizuri na wachezaji wote wapo tayari kuivaa Congo Brazavile.
Aidha Nahodha wa Timu  hiyo Bw. Issa Abdi Makame mbali na kuishukuru Serikali kwa motisha inayotoa ameahidi kujituma zaidi kwa kushirikiana na wenzake na   kufuata maagizo kutoka   Bechi la ufundi  ili kuhakikisha wanapata ushindi.
“Tunashukuru sana kwa motisha mnayotupa na sisi hatutawaangusha tutajituma kadri ya uwezo wetu tupate ushindi  ili tusonge mbele zaidi ” Aliongeza Nahodha Makame.
Timu  hiyo ya vijana chini ya  umri wa Miaka kumi na saba (Serengeti Boys) inashiriki kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana yatakayofanyika nchini Madagascar mwaka 2017.

0 maoni:

Chapisha Maoni