Posted by Esta Malibiche on Sept17.2016 in KITAIFA |
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira(katikati) katika Jukwaa akipokea Salaam ya heshima kutoka kwa
Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza kozi Na. 22
ya Mwaka 2016(hawapo pichani) katika hafla ya kufunga Mafunzo hayo leo
Septemba 16, 2016 Chuo cha Magereza, Kiwira Mbeya. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
akikagua Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza kozi
Na. 22 ya Mwaka 2016.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
akimvisha cheo cha Koplo wa Jeshi la Magereza Askari Mhitimu wa Mafunzo
hayo kwa niaba ya wenzake.
Kamishna
Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kushoto) katika jukwaa kuu
na Mgeni rasmi wakifuatilia maonesho mbalimbali ya kujihami askari kama
wanavyoonekana katika picha.
Gwaride la Wahitimu likipita mbele ya jukwaa kwa heshima
Paparazi: Baadhi ya Askari wa Jeshi la Magereza wakichukua matukio mbalimbali kutoka Uwanja wa gwaride kama wanavyoonekana.
Onesho
la kijasiri kama inavyoonekana katika picha ambapo mwendesha pikipiki
ameweza kupita kwa juu usawa wa tumbo huku askari hao wakiwa wamejilaza
chini bila uoga.
Wahitimu
wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza kozi Na. 22 ya Mwaka 2016
wakishangilia kwa makofi mara baada ya kufungwa rasmi mafunzo hay oleo
Septemba 16, 2016.
Kamishna
Jenerali wa Magereza, CGP - John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi
kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kutoa hotuba yake ya kufunga rasmi kwa
Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza katika Chuo cha Magereza, Kiwira
Mbeya. Picha zote na Lucas Mboje wa Magereza.
0 maoni:
Chapisha Maoni