Posted by Esta Malibiche on Sept26.2016 in NEWS
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akitoa hotuba ya ufunguzi wa
Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani alioizindua Kitaifa
mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki
Ajali, Tunataka Kuishi”. Katika hotuba yake, Masauni aliwaagiza Wakala
wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika
Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama
barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Askari
wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka Makao Makuu, Koplo Faustina
Ndunguru wakati alipokuwa anatoa maelezo jinsi magari mbalimbali
yanavyovunja sheria za barabarani. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa
maonyesho hayo yanayofanyika Kitaifa mjini Geita, Mhandisi Masauni
aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote
yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata
sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiyaangalia
maandamano ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo yanafanyika
Kitaifa katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita, yalipokuwa
yanaingia katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuadhimisha wiki hiyo.
Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta
yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini
kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimpa zawadi ya
Kombe la Ushindi wa kwanza Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge jijini
Dar es Salaam, Veronica Innocent, ambaye alishinda nafasi ya kwanza
katika uchorani wa picha zinazoonyesha usalama barabarani ambayo
zilipambanishwa katika shule za Mkoa wa Dar es Salaam na Geita. Masauni
aliyazindua Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, ambayo
yanafanyika Kitaifa, katika Viwanja vya CCM Kalangalala, mjini Geita.
Masauni katika hotuba yake aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini
(TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na
aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili
kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama
Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga akizungumza katika
maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayofanyika Kitaifa
katika Viwabya vya CCM Kalangalala mjini Geita. Maadhimisho hayo
yalizinduliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad
Masauni (kulia).
Washiriki wa maonesho (waendesha
bodaboda) wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa
Usalama Barabarani iliyozinduliwa katika Viwanja vya CCM Kalangalala,
mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki
ajali tunataka kuishi salama”. Maadhimishjo hayo yalinduliwa na Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni. Katika
hotuba yake Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS)
kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva
wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za
kizembe.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi cheti cha
ushiriki, Mwakilishi wa Kampuni ya Bia nchini (TBL), Amanda Walter. toa
hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani alioizindua Kitaifa mjini Geita leo. Kauli mbiu ya
Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki Ajali, Tunataka Kuishi”. Katika
hotuba yake, Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS)
kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva
wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za
kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 maoni:
Chapisha Maoni