Posted by Esta Malibiche on Sept 25.2016 in NEWS
Mkuu wa msafara wa Shirika la
Kiristo la Kuhudumia Wakimbizi Tanganyika (TCRS) Jasmine Gwamsy
akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu
vifaa vyenye thamani ya jumla ya Sh. milioni 60.92 ikiwa ni mchango wao
wa kuwafuta machozi wanakagera baada ya kuathiriwa na tetemeko la ardhi.
………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba.
Shirika la Kiristo la Kuhudumia
Wakimbizi Tanganyika (TCRS) limechangia vifaa vyenye jumla ya Sh.
milioni 60.92 ikiwa ni mchango wao wa kuwafuta machozi wanakagera baada
ya kuathiriwa na tetemeko la ardhi.
Katika kuhakikisha hali za
wananchi na ttaasisi za kutolea huduma za kijamii zinaimarika na kurudi
kwenye hali ya kawaida, wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi bado
michango yao inahitajika.
Akikabidhi mchango huo, Mratibu
wa Miradi inayoendeshwa na TCRS Oscar Rutenge pamoja na Jasmine Gwamsy
wametaja mchanganuo wa msaada huo kuwa ni pamoja na blanketi, 1680,
mashuka 840, ndoo za kutumia 840, nguo za kutumia kwawanawake, wanaume
na watoto box 50, sabuni katoni 1680 pamoja na vifaa vingine 2250.
Akipokea msaada huo Mkuu wa Mkoa
wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu amemelishukuru shirika hilo
kwa mchango wao huo kwani ni wa thamani hasa baada ya tetemeko hilo
kuwaaathiri wananchi wa mkoa huo.
Aidha, Meja Jenerali Mstaafu
Kijuu amewakaribisha na kuwataka wadau wengine waguswe kwa namna ya
kipekee na waendelee kutoa michango yao waweze kuwasaidia wananchi na
kurudisha hali yao na kuendelea na shughuli zao za kijamii na
kimaendeleo.
0 maoni:
Chapisha Maoni