Posted by Esta Malibiche on Sept 29.2016 in NEWS
Na Abushehe Nondo,Maelezo.
ASILIMIA 80 ya Watanzania
wamesema juhudi za maendeleo hazina budi kupewa kipaumbele baada ya
uchaguzi na kukataa mikutano ya kisiasa ambayo wanadai hukwamisha
shughuli za maendeleo.
Taarifa ya utafiti huo
iliyotolewa leo Jijini Dar es Salaaam na Shirika la Utafiti la TWAWEZA
ilisema kuwa utafiti huo umebeba maoni ya wananchi kuhusu demokrasia,
udikteta na maandamano nchini Tanzania.
Aidha taarifa hiyo iliongeza kuwa
takwimu za muhtasari huo zinatokana na na utafiti wa sauti za wananchi
ikiwa ni moja ya programu za Twaweza.
Pia katika utafiti huo, wataalamu
hao waliweza kubaini kuwa asilimia 49 ya wananchi wanakubaliana na
kuzuiwa kwa mikutano ya vyama vya siasa kutokana na kwamba huvuruga
umakini wa Serikali na Wananchi.
Katika suala la kumhusisha Rais
Maguli na udikteta utafiti huo umebaini kuwa asilimia 58 ya Watanzania
wanapinga uwepo wa udikteta katika serikali ya awamu ya Tano ya Rais
John Magufuli.
Aidha utafiti huo wa Twaweza pia
umebainisha kuwa asilimia 50 ya wananchi wamesema hakuna uwezekano wa
wao kushiriki kwenye maandamano yoyote.
Kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli
kuzuia mikutano ya hadhara utafiti huo unaonyesha kuwa asilimia 60
wanamuunga mkono Rais katika kuzuia mikutano ya hadhara ya kisiasa.
Utafiti huo wa Twaweza umekuja
baada ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli
kujipatia pongezi nyingi kwa jitihada zake za kupambana na na vitendo
vya rushwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni