Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya za Uvinza na
ile ya Buhigwe na kutembelea Hospitali na vituo vya Afya ndani ya Mkoa
huo wa Kigoma.
Akiwa
katika kituo cha Afya cha Uvinza, Naibu Waziri ameweza kubaini
mapungufu mbalimbali huku na kutoa maagizo kwa wasimamizi wake
kuhakikisha wanafanyia marekebisho kasoro hizo kwa muda unaotakiwa kabla
ya kuchukuliwa wahusika.
Miongoni
mwa kasoro alizobaini ni pamoja na kuwa kituo hicho licha ya kuhudumia
wananchi kama Hospitali ya Wilaya ya Uvinza, hadi sasa hakina sifa
hiyo kwani hakina Chumba cha upasuaji, Maabara hisiyofuata utaratibu
pia kutokuwa na maji kwa kituo hicho maji ambayo wanategemea kutoka kwa
wagonjwa.
“Kituo
cha Afya Uvinza, kinahudumia eneo lenye watu zaidi ya 59,000. Walipaswa
kuwa 10,000 tu. Hakina maji, umeme Kwa sababu zisizo za kawaida. Hakuna
Chumba cha upasuaji (Theatre), maabara ya kusuasua na dawa si za
kutosha.
Nimewaagiza
ndani ya miezi mitatu wawe wamekarabati eneo nusu la wodi ya wanaume
kiasi cha kuweka Chumba cha Upasuaji. Pia wavute maji na kuweka
matenki juu ili kuepukana na tabia ya kuagiza wajawazito kuja na ndoo za
maji kituoni!. Nimewapa mwezi mmoja ili wavute umeme na kuanza kutumia
Vifaa vyao Vya maabara.” Amesema Dk.Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo
yake hayo kwa viongozi wa Serikali na wa Hospitali hiyo.
Aidha,
kwa upande wa ziara yake katika Wilaya ya Buhigwe, Dk. Kigwangalla
alipongeza juhudi za wabia binafsi kwa kuweza kushirikiana na Serikali
kwenye jambo la maendeleo huku akiwahakikishia uongozi wa Hospital ya
Wasabato ya Heri Mission iliyopo eneo la Manyovu kuwa juhudi zao
wanazitambua na suala la kuifanya Hospitali hiyo kuwa Hospitali teule ya
Wilaaya zinashughulikuwa huku akiwataka kuzingatia sheria mbalimbali na
mambo madogomadogo.
Dk.
Kigwangalla ameutaka uongozi wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanafanyia
marekebisho ya barabara inayoingia Hospitalini humo pamoja na
kuhakikisha wanajenga vituo zaidi vya Afya ili kuwafikia wananchi wake.
Dk. Kigwangalla yupo Mkoani hapa kwa ziara ya siku ambapo pia atatembelea Hospitali na vituo vya Afya vya Kigoma Mjini.
(Picha zote na Andrew Chale,Kigoma)
0 maoni:
Chapisha Maoni