Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kukabidhi
kikombe kwa washindi katika mchezo wa kirafiki baina ya Wabunge
mashabiki wa Yanga na Simba ambapo Yanga wameifunga simba 5- 2
Katika mchezo huo Jumla ya Tsh
187 Million zimepatikana ambazo zitakabidhiwa rasmi kwa waziri mkuu ili
kuwasilishwa kwa wahanga wa Tetemeko la Ardhi lililotokea mjini Bukoba
mkoani Kagera likipoteza maisha ya wananchi 17 na kujeruhi wengine wengi
na kuharibu nyumba na miundo mbinu.
Mwenyekiti wa timu ya wabunge Mh.
William Ngeleja akizungumza jambo mara baada ya mchezo huo uliofanyika
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikabidhi kikombe kwa wabunge
mashabiki wa timu ya Yanga kwenye uwanja wa taifa leo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde wakati
akiwapongeza wabunge mashabiki wa Yanga kwa ushindi mnono wa magoli
5-2 dhidi ya Wabunge mashabiki wa Simba kwenye uwanja wa Taifa leo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akisalimiana na MWIGULU Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani, wakati
akiwapongeza wabunge mashabiki wa Yanga kwa ushindi mnono wa magoli
5-2 dhidi ya Wabunge mashabiki wa Simba kwenye uwanja wa Taifa leo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikabidhi kombe kwa wabunge
mashabiki wa timu ya Yanga mara baada ya ushindi wao dhidi ya wabunge
mashabiki wa timu ya Simba kwenye uwanja wa Taifa leo.
Wabunge Mashabiki wa Yanga wakishangili na kombe lao mara baada ya kuibuka washindi wa mchezo huo leo kwenye uwanja wa Taifa.
Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai
akiwavisha nishani wabunge mashabiki wa Simba mara baada ya mchezo huo
kumalizika kwenyew uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
0 maoni:
Chapisha Maoni