Afisa
Mawasiliano wa TBL Group, Amanda Walter akipokea cheti cha udhamini
wa wiki ya Usalama Barabarani kwa niaba ya kampuni kutoka kwa Naibu wa
Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni,kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki
ya Nenda kwa usalama barabarani iliyofanyika mkoani Geita.Wengine
pichani (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Geita,Ezekiel Kyunga na (Kulia) ni
Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani cha Jeshi la Polisi Kamanda
Mohamed Mpinga.
………………………………………………………………….
-Huduma za kupima afya ya Zahanati Mwendo yavutia wengi
Kampuni ya TBL Group imetunukiwa
cheti kutokana na mchango wake mkubwa katika kuendesha kampeni za
Usalama barabarani nchini ikiwemo kudhamini Wiki ya Nenda kwa Usalama
barabarani mwaka huu ambayo imezinduliwa kitaifa mkoani Geita.
Cheti hicho kutoka serikali
kilitolewa na Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni, ambaye
alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyojumuisha viongozi na
watumishi wa serikali wakiwemo wawakilishi kutoka makampuni na taasisi
mbalimbali zisizo za kiserikali.
Akiongea baada ya hafla
hiyo,Afisa Mawasiliano ya Nje wa TBL Group,Amanda Walter,alisema kuwa
TBL Group imekuwa mstari wa mbele kuendesha kampeni za Usalama
Barabarani na kudhamini Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani na
itaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine katika kufanikisha
kampeni hizi kwa lengo la kupunguza matukio ya ajali nchini.
“Mwaka huu mbali na kutoa stika
na vifaa vingine vya uhamasishaji tunalo gari maalumu la kupima afya za
madereva bure ambalo liko hapa Geita na litaendelea kuzunguka sehemu
mbalimbali nchini kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.Natoa wito kwa madereva
kujitokeza kupima afya zao na kupatiwa matibabu”.Alisema Walter.
Aliongeza kuwa mbali na kupima
afya za madereva kampuni imeandaa mafunzo mbalimbali endelevu kwa ajili
ya masuala ya usalama kwa wafanyakazi wake na makundi mbalimbali
kwenye jamii ikiwemo mafunzo ya kuhamasisha unywaji kistaarabu lengo
kubwa likiwa ni kuleta mabadiliko kwa watumiaji wanaotumia vinywaji
vyenye kilevi wasiathirike kwa kutumia vinywaji na kuleta athari
nyinginezo zitokanazo na ulevi kama vile ajali za barabarani.
Amanda pia alisema kuwa kampuni
kutokana na kutekeleza na kuzingatia kanuni za usalama hivi karibuni
ilishinda tuzo mbalimbali za usalama moja wapo ikiwa tuzo ya usalama
sehemu za kazi inaotolewa na taasisi ya OSHA ambapo pia ilishinda tuzo a
kimataifa ya Usalama ijulikanayo kama NOSA.
Wakati huohuo, gari la kupima
afya za madereva la zahanati mwendo limekuwa moja ya kivutio kikubwa
katika uzinduzi wa kampeni za Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani
ambapo madereva wengi na wananchi walijitokeza kwa ajili ya kupima afya
zao na kupatiwa matibabu.
Baadhi ya wananchi waliofika
kwenye uwanja wa Geita na kushuhudia huduma za upimaji wa afya kwa
madereva wameipongeza TBL Group kwa kuanzisha huduma hii ambayo
itawawezesha madereve wengi kupima afya zao “Unajua madereva tumekuwa
hatuna muda wa kwenda katika vituo vya afya kupima afya ila kwa njia hii
ya basi linalotembea tutafikiwa wengi”.Alisema Josephat Ngosha dereva
wa malori na mkazi wa Geita mjini.
0 maoni:
Chapisha Maoni