Jumatatu, 13 Juni 2016

MJUE LEONCE MULENDA ALIYEWANIA KUGOMBEA URAIS 2015

‘Alikula sahani moja’ na vigogo kuwania Urais na Uspika wa Bunge 2015
Ni msomi wa Shahada ya uzamivu (PhD) katika masuala ya usimamizi wa Biashara
Asema Dk. Magufuli atarejesha nchi katika misingi ya Mwalimu Nyerere

NA BASHIR NKOROMO
…………………………….
Baada ya Uchaguzi Mkuu uliofayika mwezi Oktoba, 2015, na kuiacha Tanzania ikiwa na Rais wa awamu ya tano, ambaye ni Rais Dk. John Pombe Magufuli, yapo mambo mengi yamebaki katika kumbukumbu za Watanzania walio wengi.
Kwa upande wa mchakato ndani ya CCM wa kuwapata wagombea kwenye nafasi hizo, yapo mengi ya kukumbukwa, lakini mojawapo ni majina ya waliokuwa mstari wa mbele katika vinyang’anyiro katika nafasi mbalimbali vilivyokuwa katika Uchaguzi huo Mkuu, ikiwemo kinyang’anyiro cha Urais, Makamu wa Rais, Uspika, Wabunge/ Wawakilishi na madiwani.
Walioshiriki katika kinyang’anyiro hicho wamebaki katika kumbukumbu za vichwa vya Watanzania kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo namna walivyokuwa wakionyesha ushiriki wao katika kuomba nafasi wanazoziomba kugombea kwa tiketi ya CCM, baadhi yao wakiwa vigogo na wengine ikiwa ni mara yao ya kwanza kuwania uongozi wa juu nchini.
Bila Shaka, Kijana Leonce Mulenda ni miongoni mwa wanachama wa CCM wanaokumbukwa  kutokana na umahiri alioonyesha wakati akishiriki katika kinyang’anyiro hicho.

Kwa waliofuatilia kwa karibu kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya urais na Uspika wa Bunge, ndani ya CCM watakubali kwamba  Mulenda mwenye umri wa miaka 44, ni kijana anayeonyesha ari, utashi na hamu kubwa ya kutaka kuwatumikia Watanzania katika kulijenga Taifa.
Katika harakati zake za kuonyesha ari, utashi na hamu ya kutaka kuwatumikia Watanzania, wakati wa vuguvugu hilo la Uchaguzi Mkuu uliomalizika mwaka jana wa 2015, Mulenda ni miongoni mwa Wanachama wa CCM, walioingia kwa kasi kubwa  katika kinyang’anyiro cha kuomba kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM.

0 maoni:

Chapisha Maoni