Tarehe 16 Septemba, 2016 saa 3:00 asubuhi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(pichani) anatarajia kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza Chuo cha Magereza Kiwira, Tukuyu – Mbeya.
Mafunzo hayo yalilenga kuwaandaa
askari hao kuwa viongozi wasimamizi wa kazi za kila siku zinazopaswa
kufanywa na viongozi wa ngazi hiyo Magerezani.
Sherehe hizo zitajumuisha mambo yafuatayo :-
- Mgeni rasmi kukagua Gwaride rasmi lililoandaliwa na wahitimu hao;
- Mgeni rasmi kutoa vyeti vya sifa kwa wanafunzi waliofanya vizuri na
kumvisha cheo mwanafunzi mmoja kwa niaba ya wahitimu wengine na;
- Mgeni rasmi kutoa hotuba.
Sherehe za ufungaji wa mafunzo
hayo zinatarajia kukamilika saa 8:00 mchana. Vyombo vya Habari
vinakaribishwa kwenye sherehe hizo tarehe 16 Septemba, 2016 kuanzia saa
3:00 asubuhi.
Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mrakibu Msaidizi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
15 Septemba, 2016.
0 maoni:
Chapisha Maoni