Posted by Esta Malibiche on Sept29.2016 in NEWS
Mbunge
wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka akionesha tuzo ya kimataifa
(UN) ya Maendeleo Endelevu ya Mwana Mfalme Khalifa Bin Salman Al Khalifa
aliyotunukiwa hivi karibuni New York Marekani wakati akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo.
Profesa Anna Tibaijuka akionesha cheti alichokabidhiwa sanjari na tuzo hiyo.
Profesa Tibaijuka akisisitiza jambo katika mkutano huo na wanahabari. Kulia ni Mratibu wa mkutano huo, Mussa Ally.
wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
MBUNGE
wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka amekacha kuchukua dola 300,000
alizopewa baada ya kutunukiwa tuzo ya Maendeleo Endelevu aliyopewa na
Umoja wa Mataifa (UN), kutokana na sakata la fedha za Escrow Tegeta.
Tuzo
hiyo aliipokea Septemba 23 mwaka huu New York Marekani ambayo mfadhili
wa tuzo hiyo ni wa waziri mkuu wa Bahrain mwana mfalume Khalifa bin Al
Khalifa.
Akizungumza jana Dar es Salaam Profesa Tibaijuka alisema kwa sasa umoja
wa mataifa umeingia katika awamu ya pili ya maendeleo, ambao umekuja
kupisha yale malengo 17 ya mileniam ambayo yote yeye alikuwepo, hivyo
aliokuwa wanatoa tuzo walinona kwa namna alivyoshiriki kwa kiasi
kikubwa.
"Tuzo hizi si za kuomba, ni watu wanakaa na kupendekeza mtu wa kupewa,
na hii ni mara ya pili, mara ya kwanza nilipewa mwaka 2009 nchini
Swideni," alisema na kuongeza.
"Tuzo zinatoka kwa niaba ya jamii inayotoka au kuitumikia na kufanya
nayo kazi, hivyo wamatambua mchango wangu katika kuwatumikia wananchi wa
Muleba," alisema.
Aidha Profesa tibaijuka alitaja sababu zilizpokekea yeye kutochua dola 300,000 za Marekeni za tuzo hiyo.
"Sikuichukua kwa sababu ya yaliyonikuta hapo mapema, kulikuwa na
uwezekano wa kuichukua lakini nikasema kwa hali halisi ya nyumbani,
hatuna sheria ya kupokea tuzo, michango na zawadi kwa hiyo mimi nikaicha
mezani wao wafanye wanayotaka," alisema na kuongeza.
"Unapoona mtu kama mimi nafanya kazi nakwenda kuchafulia kwenye kitu
ambacho siusiki nacho, sasa Unapoipokea hapa utaonekana kama umevunja
maadili au umejinufaisha kwa kuwa ndio mambo ya kwetu, hivyo
nikawaachia," alisema.
Aliongeza kwa sasa umeshapeleka mswada binafsi bungeni wa kuweka sheria
ya michango ili vitu vya hiari kama hivi vinapokuja katika jamii
visimamiwe na si kupotoshwa kisiasa.
"Kwa maana jambo hili halina kificho, yaani huwezi kumzungumzia Anna
Tibaijuka bila kutaja suala la Escro, hayo hayakwepeki kwa sababu
yalitengenezwa yakawa hivyo, mtu asiyehusika anavalishwa joho lisilo
muhusu.
"Lakini kwa sababu jamii haina uwezo wa kuchimba chini, unabaki kuwa
uongo na kushindwa kujua ukweli umesimama wapi, lakini wao (UN) wanajua
hii ni propanda la sivyo nisingesimama hapa na tuzo," alisema.
Aliongeza licha ya yeye kuwa mstaafu wa umoja wa mataifa bado
wanamfuatilia katika shughuli za kimaendeleo ambazo anazifanya akiwa
ndani na nje ya nchi.
"Kama ukijikwaa, ukianguka na kusimama watu wanaangalia kulikoni, na huu
ni utamaduni wao, kwa hiyo pale uongo na fitina havina nafasi," alisema
kwa msisitizo wakati akizungumza na wanahabari.
Diwani wa Kata ya Karambi ambaye pia ni Mjumbe wa mkutano Mkuu wa Taifa
wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Felix Bwahama ambaye
aliongozana na Profesa Tibaijuka alishukuru UN kwa kumtunuku tuzo hiyo
ambapo alisema ni fahari kwa wanakagera na taifa kwa ujumla licha ya
baadhi ya watu nchini kubeza kazi anazizifanya ambazo zinaonekana
kimataifa.
0 maoni:
Chapisha Maoni