Mashindano
maarufu ya Mrembo wa Gereza katika Gereza la Lang’ata yamelenga
kuwasaidia wafungwa wakike kupata afueni ya kisaikolojia na kurudi
katika hali zao za zamani kabla ya kifungo.
Shindano
hilo la urembo limelipa gereza la Lang’ata umaarufu mkubwa baada ya
video za mashindano hayo kurushwa katika mitandao ya kijamii mbalimbali
duniani.
Katika
mashindano hayo ya mrembo wa gereza Mtanzania Tina Martin ameshika
nafasi ya pili ya taji la mrembo wa Gereza akipitwa kwa spidi ya mwendo
kasi na mwanadada wa Kikenya Ruth Kamande.
Mrembo wa Tanzania kwenye gereza hilo, Tina Martin akiwa kwenye pozi
Mtanzania
huyo amehukumiwa kifungo katika Gereza hilo baadaya kukutwa na tuhuma
za kuingiza madawa ya Kulevya kwa njia za magendo nchini Kenya.
Ruth
Kamande amewapiku washindani wenzake 19 na kutwaa taji la mrembo wa
Gereza la Lang’ata , mashindano ambayo yanafanyika kila mwaka gerezani
hapo.
Ruth
Kamande ni binti wa Kikenya mwenye umri wa miaka 21 ambaye alihukumiwa
kwenda jela kwa kosa la mauaji ya mpenzi wake bwana Farid Mohammed.
Bi
Ruth alifanya tukio hilo nyumbani alipoishi na mpenzi wake eneo la
Buruburu Jijini Nairobi mnamo mwaka 2015, baada ya kuona kile
kinachodaiwa kuwa ni ujumbe wa kimapenzi kwenye simu ya mpenzi wake
kutoka kwa mwanamke mwingine (Mchepuko).Bw Farid alipoteza maisha akiwa
anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta –KNH.
Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC).
Tazama hapa kushuhudia tukio hilo:
0 maoni:
Chapisha Maoni