Marekani imemrudisha nyumbani msomi mmoja wa Rwanda anayetuhumiwa kuwa mtu muhimu katika mauaji ya kimbari ya 1994.
Kufurushwa kwa Leopold Munyakazi kunajiri baada ya kupoteza kesi ya kupata uhifadhi nchini Marekani.
Anatuhumiwa
kwa kuvaa majani ya mgomba wakati wa mauaji hayo ya kimbari ili
kujitambulisha kuwa raia wa kabila la Hutu,mbali na kupanga mashambulio
ya usiku katika nyumba za familia za watu wa kabila la Tutsi .
Bwana Munyakazi ,aliyewahi kuhudumu kama profesa wa chuo kikuu amekana madai hayo.
Takriban
Watutsi 800,000 na watu wa kablila la Hutu wenye ustani waliuawa na
wapiganaji wa Kihutu katika kipindi cha siku 100 pekee mwaka 1994.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni